Pages

Monday, June 1, 2015

PICHA YA MKE WA RAIS MPYA WA NIGERIA AKIWA NA MABINTI ZAKE

 
Mke wa Rais wa Nigeria, Mrs Buhari akiwa na mabinti zake 
SOMA ZAIDI >>> »
Blogger Tricks

Friday, May 29, 2015

SEPP BLATTER ASHINDA TENA URAIS WA FIFA

Sepp Blatter baada ya ushindi.

Blatter akiwa na mpinzani wake Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan.

SEPP Blatter ameshinda tena Urais wa FIFA kwa awamu ya tano baada ya kumshinda mpinzani wake Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan.
Blatter amepata kura 133 dhidi ya 73 za mpinzani wake huyo katika raundi ya kwanza ya kinyang'anyiro hicho kilichofanyika nchini Uswizi leo licha ya kukumbwa na skendo za ufisadi.

SOMA ZAIDI >>> »

MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA AAPISHWA NA MKUU WA MKOA WA DODOMA LEO

Mhe. Athony Mavunde akila kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Hayupo Pichani) Mei 29,2015
Mhe. Athony Mavunde akitia saini hati ya kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa Mei 29, 2015
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto) akipongezwa na baba yake mzazi Ndg. Peter Mavunde mara baada ya kula kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya Mei 29,2015
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto kwake) na wajumbe wa kamatiya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma wakati wa Hafla ya kumuapisha Mkuu huyo mpya wa Wiaya ya Mpwapwa Mei 29,2015
SOMA ZAIDI >>> »

MAGAZETI YA KITANZANIA YA LEO IJUMAA MAY 29,2015






SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, May 28, 2015

MAAFISA WA FIFA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Maafisa saba wa juu wa shirikisho la soka duniani, FIFA wamekamatwa kwa shutuma za kupokea rushwa. Maafisa hao walikamatwa kwenye hoteli ya Baur au Lac ya jijini Zurich, Jumatano hii. Polisi wa Uswisi wamekamata maafisa hao wakiwemo makamu wa rais wawili baada ya kuivamia kwa kushtukiza hoteli hiyo.
 Makamu wa rais wa FIFA, Jeffrey Webb anaaminika kuwa mmoja wa maafisa waliokamatwa alfajiri ya leo wakiwa kwenye hoteli ya kifahari nchini Uswisi
 
Eduardo Li, kutoka Costa Rica naye pia alikamatwa kwenye hoteli hiyo ya kifahari 
Hatua hiyo imekuja kufuatia upelelezi uliofanywa na Marekani kwa kipindi cha miaka mitatu. Waendesha mashtaka wa Marekani wametoa hati za kukamatwa kwa maofisa 14, kwa madai yakiwemo kutakatisha fedha haramu, ulaghai na mengine.
Madai hayo ni pamoja na maafisa wa FIFA kupokea rushwa ifikayo dola milioni 150.
Mamlaka za Uswisi zimefungua upelelezi tofauti wa jinai katika utendaji wa FIFA kuhusiana na nafasi za kuandaa makombe ya dunia ya mwaka 2018 na 2022 zilizoenda kwa Urusi na Qatar.
Rais wa FIFA Sepp Blatter si miongoni mwa wanaoshtakiwa lakini alikuwa mmoja wa maafisa waliokuwa wakichunguzwa.

Uchaguzi wa FIFA utaendelea kama ulivyopangwa Ijumaa hii na pia michuano ya kombe la dunia nchini Urusi na Qatar haitaathirika.
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, May 14, 2015

PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAZISHI YA MTOTO WA BABA WA TAIFA

 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila akisali mbele ya jeneza la marehemu John Guido Nyerere kabla halijaingia kanisani kwa ajili ya ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama.
 Viongozi na wananchi wakishiriki ibada ya kumuombea marehemu John Gaudo Nyerere katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama
 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila
akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Guido Nyerere baada ya kukamilika kwa ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki
la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya
Butiama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere yaliyofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa ,Butiama.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu John Guido Nyerere likiteremshwa kaburini na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
 Mama Maria Nyerere akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akiweka udongo kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Mtoto wa mwisho wa marehemu John Guido Nyerere anayefahamika kwa jina la Wanzagi akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na shangazi yake Anna Nyerere.

 Ni huzuni kwa kila mtu.
 Mama Maria Nyerere akiweka shada la mau kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Mtoto wa Marehemu anayeishi Lusaka Zambia, Sofia Nyerere Mwape akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yake marehemu John Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima mbele ya kaburi la marehemu John Gaudo Nyerere mara baada ya kuweka taji la maua.
 Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu John Nyerere kwenye mazishi yaliofanyika nyumbani kwa marehemu Baba wa Taifa Butiama.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishiriki kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Baadhi ya Watoto wa marehemu pamoja na ndugu wengine.
 Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akisoma salaam za rambi rambi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wakati wa mazishi ya John Nyerere.
Emily Magige Nyerere akifafanua jambo wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere.
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, May 6, 2015

SALMAN KHAN AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO KWA MAUAJI


Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan (katikati).

Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa mjini Mumbai.
Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo.
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Jaji wa mahakama hiyo, Khan anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Credit: BBC
SOMA ZAIDI >>> »