Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza Mkataba wake.
“Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,” amesema Kavumbangu akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya kusaini Mkataba huo ambao unamfanya alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.
Pamoja na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki kwa miaka miwili aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye kumbukumbu zake kwa ameshinda nayo mataji.
![]() |
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.
![]() |
Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu la penalti.


No comments:
Post a Comment