Rwanda imeanza rasmi wiki moja ya maombolezo
kukumbuka miaka 20 tangu kutokea kwa mauji ya kimbari. Rais Paul Kagame
aliwasha mwenge ambao utawaka kwa siku 100 – muda sawa na mauaji
yalivyodumu.

Rais
Paul Kagame wa Rwanda na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
wakiwasha kwa pamoja mwenge utakaoendelea kwa siku 100 kukumbuka mauaji
hayo ya mwaka 1994.

Waziri
Mkuu mstaafu wa Uingereza, Tony Blair na Rais mstaafu wa Afrika Kusini
Thabo Mbeki ni miongoni mwa wageni mashuhuri kutoka nje ya Rwanda
waliohudhuria shughuli hiyo. Hapa wakiweka shada la maua.

Machafuko
ya mwaka 1994 yalidumu kwa siku 100, watutsi na wahutu wenye msimamo
takriban wa kadri 800,000 wapatao waliuawa katika mapigano hayo ya
kikabila.
Mzozo wa kidiplomasia umezuka baina ya Rwanda na Ufaransa na hata umesababisha balozi wa Ufaransa nchini humo, Michel Flesch, asihudhurie shughuli hizo.
Wengi wa walioathirika walikatwa kwa mapanga katika mauaji yaliyoanza 6 Aprili 1994, muda mfupi baada ya Rais Juvenal Habyarimana ambaye alikuwa mhutu kuuawa wakati ndege ilipotunguliwa katika anga ya mji mkuu Kigali.
uko vizuri brother
ReplyDelete