Mwenyekiti
wa Umoja Asasi za Kiraia, Bw. Irenei Kiria akifafanua jambo mbele ya
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Tathimini zilizofanywa na
asasi za kiraia kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba mpya unaoendelea
katika Bunge la Katiba mjini Dodoma, Katika tahimini yao hiyo, umoja huo
umegundua madhaifu mengi sana ambayo kama hayatapatia ufumbuzi wake
basi katiba mpya yenye kumjali mtanzania ni Ndoto kupatikana. Pembeni ni
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi Kijo
Bisimba.
Baadhi ya Wanachama wa Asasi za Kiraia (AZAKI), wakifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi Kijo Bisimba akifafanua jambo.
Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko hilo.
Kila mmoja akifuatilia kwa karibu...
Tupenda
kuipongeza serikali na hasa kumpongeza kwa dhati Rais Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kukubali kuansiha mchakato wa kutunga katiba mya ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Tunalishukuru
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutunga sheria zote
zinazowezesha kuelekeza hatua mbali mbali za mchakato huu.
TUnaishukuru
Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Uongozi wa Jaji Joseph Sinde
Warioba kwa kuendesha zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa wananchi na
kuandika rasimu ya kwanza nay a pili za Katiba Mpya.
Tunawashukuru
wananchi, wataalamu na Asasi mbali mbali kwa kushiriki na kutoa maoni
katika hatua mbali mbali za mchakato huu wa kutunga Katia Mpya.
Kutokana
na namna mambo yananvyokwenda katika Bunge Maalum la kutunga Katiba,
Asasi za Kiraiaziliona umuhimu kukutana kuanzisha tarehe 8 Aprili 2014
kutafakari yanayojiri na kukubaliana utakuwa mchango wa Asasi katika
kuhakikisha Tanzania inapata katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na
ya vizazi vijavyo. Baada ya vikao vya mara kwa mara na majadiliano mengi
pamoja na kukusanya taarifa kadhaa. Hatimaye katka kikao cha tarehe 15
Aprili 2014 tulikubaliana tamko.
Kwa hiyo sisi Asasi za Kiraia tumekubaliana ya kwamba:
Kwa kuwa
huu ndiyo mchakato pekee hapa Tanzania wa kutunga katiba mpya ambao
umewahusisha wnanchi tangu hatua za awali, tunauunga mkono na kuutakia
mafanikio.
Kwa kuwa
Rais wa Jamhuri wa Tanzania amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha katiba
mpya inapatikana kabla ya kipidi chake cha uongozi kuisha, ni vema Bunge
Maalum la Katiba likazingatia yafuatayo;
1. Sisi
Asasi za Kiraia tunaunga mkono Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama
ilivyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kwa kuwa imekidhi
mahitaji ya Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo kama ikipita
itaimarisha uadilifu, uwazi, uwajibikaji, amani na umoja wetu.
2. Kwamba
hatujafurahishwa na mijadala ndani ya Bunge Maamul la Kutunga Katiba
mijadala ambayo imepoteza utaifa na badala yake imejikita kwenye
kutoheshimiana, ubabe, ubaguzi, vijembe na vitisho.
3. Kwamba
tumehuzunishwa sana na tabia ya kudhihakiana na kudharau Rasimy ya pili
ya Katiba pmoja na tume ya mabadiliko ya katiba na hasa Mwenyekiti
wake.
4.
Tunaona kwamba mwennendo wa mijadala ni kuelekea kutetea maslahi ya
watawala wa vyama vya siasa badala ya maslahi ya utaifa na ustawi wa
wananchi.
5. Kwamba
kitendo cha baadhi ya wajumbe kupendekeza kutoa maneno; uwajibikaji,
uadilifu, uwazi katika kipengele cha tunu za taifa inatia mashaka kama
nia ya Bunge Maalum la Katiba ni kutuletea katiba itakayotutatulia
matatizo hayo.
6. Kwamba
hatufurahishwi na malumbano yasiyo na tija yanayochukua muda mrefu
kwenye mambo madogo madogo. Hii inapelekea kupoteza muda na hivyo
kutumia rasilimali za umma vibaya.
7. Kwamba
hatujafurahishwa na kufungwa kwa tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba. Na pia hakuna juhudi za serikali kuwafikishia wananchi Rasimu ya
Katiba mpya na kuwaelimisha maudhui yake.
8.
Tumeelewana kwamba tulikosea kutuga sheria inayohusu wabunge wa
kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la katiba. Kwa kawaida
watatetea maslahi yao kwanza kabla ya maslahi ya wananchi. Mfano bunge
la Tanzania lina wabunge 357, lakini rasimu inapendekeza wabunge 75 tu.
Hili ni tishio la wazi kwa maisha ya kisiasa ya baadae ya wabunge
madalakani sasa na hivyo wanapata umoja wa kupambana kuhakikisha rasimu
hii isipate ka ilivyo.
9.
Tunaelewa pia kwamba, Rasimu hii imependekezwa kupunguza madaraka ya
Rais ya kuteua viongozi na watendaji wa serikali. Jambo hili, kwa
mtazamo wetu ni tishio kwa wagombea urais kwamba hawatakuwa na nguvu ya
kuahidi wapambe wao nafasi za uteuzi ili wawaunge mkono kwenye kampeni
ya uchaguzi.
Rai yetu Umoja wa AZAKI.
Tunasihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Uongozi wa Bunge hilo kurekebisha hizo kasoro walizozieleza.
Irenei Kiria
Mwenyekiti wa Umoja wa Asasi za Kiraia (AZAKI).
No comments:
Post a Comment