Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara
( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia
ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa
Rais wa China Li Yunchao na wa mwisho kushoto
ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.
Gari la kisasa la kurushia matangazo ya
moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikagua ndani ya Gari la kisasa la kurushia
matangazo la TBC mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Pichani baadhi ya Screen zikionyesha
picha mbalimbali za matukio yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja wakati wa hafla
ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC
lililopatikana kwa msaada wa Serikali ya China.
: Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la
kurushia matangazo la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia
matangazo Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Bw. Clement Mshana mara baada ya gari hilo
kukabidhiwa na kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua
gari la kurushia matangazo la TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni
Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Waziri wa Nchi ofisi
ya Rais Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC
Clement Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya Makumu wa Rais wa China Li
Yunchao na Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za
Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China Li Yunchao akiangalia picha zinazoonyesha vipindi vinavyorushwa na
Startimes alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Msafara
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao ukiwasili
katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC)
alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la
kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China
jana jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akisalimiana na baadhi
ya Wafanyakazi wa Startimes na TBC mara baada ya kuwasili katika Viwanja
vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipokuwa mgeni rasmi
katika hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB
Van) leo jijini Dar es Salaam.Gari hilo limetolewa kwa Msaada wa
Serikali ya China.Katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo wa Tanzania Dkt. Fenella Mukangara.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akijadiliana na jambp na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Startimes Bw. Jack Zhou.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Bw. Assah Mwambene (katikati) wakati wa hafla ya makabidhiano na
uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja (OB
Van) ambalo Serikali ya China ili kutoa msaada kwa Shirika la Utangazaji
la Taifa (TBC). Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akitoa
hotuba wakati wa hafla fupi ya makabidhiano na uzinduzi wa gari la
kurushia matangazo(OB Van) la Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) leo katika viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
: Katikati Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwa na wake Makamu wa Rais wa
China Li Yunchao kushoto kwa Waziri Fenella katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Serikali na wafanyakazi wa TBC na Startimes. Picha na Frank Shija. WHVUM















No comments:
Post a Comment