Pages

Monday, July 28, 2014

MANISPAA YA KINONDONI YAWAFUKUZA KAZI WATUMISHI WAKE

Baraza  la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limewafukuza kazi watumishi wake tisa na kuwapa onyo wengine wawili kutoka Idara tofauti kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya Utoro kazini, Matumizi mabaya ya madaraka na ofisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana  jijini Dar es salaam na afisa habari wa Manispaa hiyo Sebastian  Mhowera , hatua hiyo imefuatia kikao kilichofanyika julai 22 mwaka huu chini ya Mstahiki Meya Yusuph Mwenda.

Amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine baraza hilo lilijadili na kutolea maamuzi  mashauri ya mashtaka ya nidhamu yaliyofunguliwa kwa watumishi 11 wa Idara mbalimbali za Manispaa hiyo.

Kati ya Watumishi 11 waliofunguliwa Mashtaka, watumishi 6 ni wa Idara ya Afya, 2  wa Idara ya Elimu ya Sekondari ,  3 ni wa Idara ya Utawala na Utumishi ,  Maafisa  watendaji wa Mitaa  2 na polisi msaidizi 1.                                 

Mhowera amesema  Baraza  hilo la Madiwani manispaa ya kinondoni limewataka watumishi wote  kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na maelekezo ya Serikali katika kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma kwa Umma


No comments:

Post a Comment