Pages

Thursday, July 31, 2014

MSANII MWENGINE ANASWA NA MADAWA NCHINI CHINA

Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.

HUKU modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong, China. 
JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa madawa ya kulevya nchini China.

No comments:

Post a Comment