Pages

Friday, August 8, 2014

DROO YA UEFA YAFANYIKA LEO

Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kuwa kuna timu hatari katika droo ya UEFA iliyofanyika leo ijumaa.

ASERNAL watakabiliana na Besiktas  katika mchezo wa raundi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA).
Arsene Wenger alikwepa kukutana na Athletic Bilbao, Lille , FC Copenhagen, Standard Liege, lakini sasa atachuana na timu hiyo ya Uturuki ambayo siku za karibuni ilimsajili Demba Ba kutoka Chelsea kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni  4.7.
Besiktas ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita, lakini imefuzu kucheza UEFA baada mabingwa Fenerbahce kufungiwa kucheza mechi za michuano ya ulaya kwa kosa la kupanga matokeo ya mechi ya nyumbani.
Arsenal watasafiri kwenda Uturuki kucheza mechi ya kwanza Agosti 19 au 20 mwaka huu na mechi ya marudiano itapigwa Emirates Agosti 26 au 27.
Kiungo wa Asernal mwenye asili ya Uturuki, Mesut Ozil alifurahishwa na droo na kuandika kwenye mtandao wa Twita akisema: 'Droo nzuri! tayari tunaangalia mbele kuelekea mechi dhidi! @Besiktas! #Turkey #İstanbul #Arsenal #AFC #UCLdraw'.
Wakati huo huo, leo asubuhi, Celtic wamepewa nafasi ya kusonga mbele baada ya kubainika kuwa klabu ya Legia Warsaw ilimchezesha mchezaji asiyekuwa na vigezo.
Kamati ya nidhamu ya UEFA ilikutana na kutoa maamuzi kabla ya droo mjini Nyoni na kuamua kuwa Celtic wanatakiwa kupewa ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa pili na inamaanisha wamesonga mbele kwa magoli ya ugenini.
DRAW NZIMA HII HAPA
FULL CHAMPIONS LEAGUE PLAY-OFF ROUND DRAW
Maribor vs Celtic
Red Bull Salzburg vs Malmo
Aalborg vs APOEL
Steaua Bucharest vs Ludogoret
Slovan Bratislava vs BATE
Besiktas vs Arsenal
Standard Liege vs Zenit
Copenhagen vs Bayer Leverkusen
Lille vs Porto
Napoli vs Athletic Bilbao
Ties to be played on the 19/20 and 26/27 August 

No comments:

Post a Comment