Pages

Saturday, August 2, 2014

TAIFA STARS VITANI KESHO

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kesho inashuka dimbani kucheza mechi ya marudiano dhidi ya wenyeji Msumbiji katika uwanja wa Taifa wa Zimpeto, nje kidogo ya jiji la Maputo, kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali ya mataifa ya Afrika mwakaini nchini Morocco.Taifa Stars itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita.
Katika mchezo wa kesho, Stars inahitaji ushindi wa aina yoyote ile au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili kusonga mbele hatua ya makundi.
Kocha mkuu wa Stars, Mholanzi, Mart Nooij alisema vijana wake wapo fiti kwa ajili ya mechi ya kesho na wanaweza kuiondoa timu yake ya zamani ya Msumbiji.
Kabla ya kutua Maputo jana, Taifa stars ilipitia Johannesburg nchini Afrika kusini ilipoweka kambi ya siku mbili. Kambi hiyo imeelezwa kuwa ya mafanikio kwani imewajengea imani kubwa wachezaji wa Stars.
Wakati huo huo washambuliaji wawili wa kimataifa walioshindwa kujiunga na timu nchini Afrika kusini, wanaokipiga Tp Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamewasilia asubuhi ya leo mjini Maputo tayari kwa mechi ya kesho.

No comments:

Post a Comment