Ingawa Nafasi yake katika muziki wa Bongo Fleva ilikuwa ikipanda taratibu kulingana na aina ya muziki aliokuwa akiumba,single iliyomtambulisha zaidi kwenye muziki wa Bongo Fleva inaitwa Kua uone ambayo alimshirikisha Ally Kiba.
Mchana wa leo imetoka taarifa kuwa amefariki dunia ambapo kwa zaidi ya mwezi mmoja alikua kalazwa kwenye hospitali ya Nyangao iliyopo Mkoani Lindi ambapo kiasili ndiko nyumbani kwao.
Mipango ya mazishi imepangwa ambapo atazikwa kesho huko huko Lindi,Rest In Peace Side Boy,moja ya post zake kwenye mtandao wa Facebook aliandika ‘habari za usiku huu wapendwa!dua zenu zinahitajika coz hali yangu c poa kabisa’
Side Boy Alitoa single kadhaa ikiwemo Hujafa hujaumbika,Jifungue salama,Usimdharau Usiyemjua na Kua Uone.
Chanzo: Millard Ayo
Chanzo: Millard Ayo


No comments:
Post a Comment