Pages

Tuesday, October 21, 2014

JE, SITTI MTEMVU KUVULIWA TAJI LA MISS TANZANIA 2014 LEO?


Kamati ya Miss Tanzania leo inatarajiwa kuelezea ukweli juu ya sakata la kudanganya umri la mshindi wa taji hilo mwaka huu, Sitti Mtemvu.

Mratibu wa shindano hilo Hashim Lundenga amesema kamati yake itaelelezea taarifa ambazo walikuwa nazo kuhusiana na mrembo huyo na matokeo ya uchunguzi baada ya taarifa nyingi zilizoibuka.


"Yamesemwa mengi na yameandikwa mengi, hivyo leo itajulikana kama atavuliwa taji ama la" maneno hayo amesema Lundenga

No comments:

Post a Comment