Chumba cha kompyuta cha washiriki wa Shindano la Mashujaa wa Kesho.
Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mashujaa wa Kesho wakipitia fomu zao.
ZOEZI
la uchukuaji fomu kwa ajili ya vijana mbalimbali kushiriki katika
Shindano la Mashujaa wa Kesho la Statoil limeendelea kushika kasi huku
idadi kubwa ya vijana wakiendelea kurejesha fomu kwa lengo la kushiriki
katika kinyang’anyiro hicho.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Ofisa Mawasiliano wa Statoil Tanzania,
Erick Mchome alisema hadi sasa zaidi ya vijana 150 wamerejesha fomu zao
tayari kwa kuyashindanisha mawazo anuai ya miradi yao walioiwasilisha
kwa ajili ya kushiriki katika shindano hilo.
Mchome alisema vijana hao wamejaza fomu kwa ajili ya kushiriki katika
shindano hilo kuwania kitita cha hadi Dola 5,000 kwa mshindi wa kwanza.
“Kimsingi
zoezi hili la shindano la Mashujaa wa Kesho limepokelewa vizuri na
linaendelea vizuri sana vijana wengi wa Mtwara wamejitokeza kuchukua
fomu na baadhi wameanza kuzirejesha fomu zao…zaidi ya vijana 150 tayari
wamerejesha fomu,” alisema Mchome.
Hata hivyo kiongozi huyo aliwataka vijana ambao wamechukua fomu
kuzirejesha fomu zao kwa wakati kwenye vituo walivyoelekezwa ili hatua
zingine za utaratibu wa shindano hilo ziweze kuendelea.
“Ningependa
kuwakumbusha washiriki kuwa mwisho wa kurejesha fomu ni Oktoba 10, 2014
saa nane kamili kwenye vyuo vya Naliendele Agricultural Institute,
Tanzania Institute of Accountancy, VETA, Chuo cha Utumishi na Chuo cha
Stella Maris Pamoja na Pride FM,” alisisitiza Mchome.
Akifafanua zaidi, Mchome alisema mchujo wa kupata washiriki 40
watakaoingia hatua ya pili utafanyika mara baada ya zoezi la urejeshwaji
fomu kukamilika na kutakuwa na mchujo wa tatu ambao ni wa mwisho na
kuwatoa washindi watano watakao wania dola 5,000 kwa mshindi wa kwanza
na dola 1,000 kwa wa shindi wa pili, tatu, nne na tano .
Shindano
hilo la vijana linalojulikana kama Mashujaa wa Kesho lenye lengo la
kuhamasisha ujasiriamali lilizinduliwa rasmi Septemba 3, 2014 na kampuni
ya Statoil na linatarajiwa kumalizika Desemba 12 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment