Treni hiyo iliyokuwa na mabehewa 35, ilikuwa
ikisafirisha mbolea aina ya sulphur. Kichwa cha treni hiyo kiliacha njia
na mabehewa saba kati ya 21 kutumbukia kwenye mtaro.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda,
Faraji Abduli, Seif Juma Aziza Salimu walisema mabehewa hayo yalianguka
jirani na mashamba ya wananchi yaliyokuwa yakisafishwa kwa kuchomwa
moto.
Kutokana na moto huo, mabehewa matatu kati ya saba
yaliyoanguka, yalishika moto uliosambaa kwenye mabehewa mengine mawili
na kuyateketeza.
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia baadaye zilidai
kuwa kuungua kwa mbolea hiyo kumesababisha madhara kwa baadhi ya wakazi
wa eneo la jirani kutokana na moshi kuwaumiza vifua na kusababisha
wakohoe.
Kaimu kamanda wa polisi wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi SSP Athumani Mwambalaswa alisema:
“Mabehewa 21 yamerudishwa Tazara na taarifa za tukio hilo zitatolewa na Ofisi ya Tazara Dar es Salaam.”
“Mabehewa 21 yamerudishwa Tazara na taarifa za tukio hilo zitatolewa na Ofisi ya Tazara Dar es Salaam.”
Akizungumzia madhara waliyopata wananchi kutokana
na kukohoa kulikosababishwa na moshi huo wa kuungua mbolea, Mwambalaswa
alisema wanajitahidi kuwasiliana na wataalamu wa afya ili wafike eneo la
tukio.
“Hili la watu kukohoa, siwezi kuthibitisha kwa
sasa, maana sisi siyo wataalamu wa afya hadi watakapofika wahusika,”
alisema na kuongeza: “Nimewasikia wananchi wakilalamika, lakini mambo
yote haya yatazungumzwa na ofisi Tazara na siyo Jeshi la Polisi Mkoa wa
Pwani.”
No comments:
Post a Comment