Leo, October 2, Staa wa muziki wa bongo flava Nasibu Abdul
aka Diamond anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza umri wa
miaka 25.
Mpenzi wake, Wema Abraham Sepetu ambaye huenda wengi wanasubiri
kusikia atasema nini au atatoa zawadi gani kwa Diamond ambaye alimpa
gari aina ya Nissan Murano, ameandika machache kwenye Instagram na
kueleza kuwa anajipanga kuandika ujumbe mzuri zaidi.
“Happy Birthday to you my original soul... ngoja nitulie kwanza ndo
niandike caption maana nina mengi kwa kweli... ila jua nakupenda
sana...” Ameandika Wema.
Wema sepetu siku ya Birthday yake
Tuendelee
kusubiri kitatokea nini pale Golden Jubilee Towers, Dar ambapo sherehe
ya siku ya kuzaliwa ya Diamond itafanyika na tayari wageni maalum
wameshaalikwa.
Naye Shetta ameamua kumlipa fadhira ya shukurani Diamond Platinumz
kwa mchango wake kwenye maendeleo ya muziki wake ikiwa ni sehemu ya
kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.
Shetta ameandika kwenye Instagram:
“Kwenye maisha Kila mtu ana watu wake ambao ni muhimu sanaaaa
huenda wamefanya vitu vingi,huenda ikawa ushauri au kupigania kwa njia
yoyote ile kuhakikisha mafanikio ya mtu fulani japo hata asilimia
ndogo,nisiwe muongo Naseeb katika watu ambao wamekua kwenye sehemu kubwa
katika kazi zangu na issue zingine za kawaida katika kipindi kirefu
sasa... Mimi namuonaga zaidi ya ndugu na sio rafiki tenaaa kwa vile
tulivyoishi na tunavyoendelea kuishi mpaka sasa...back 2 the point Mwaka
1989 mwezi na tarehe kama ya leo huyu jamaa Alizaliwa,so leo ni siku
yake muhimu Naomba mnisaidie kumuwish #HAPPYBIRHTDAY Mr Dangote
Inshallah M/mungu Azidi kuleta kheri na baraka nakutakia maisha marefu
#BabaQayllah cc @diamondplatnumz”
No comments:
Post a Comment