Pages

Friday, March 13, 2015

VIINGILIO MECHI YA YANGA SC DHIDI YA FC PLATNUM VYATAJWA

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ametoa taarifa ya viingilio kwa mchezo wa keshokutwa dhidi ya FC PLATNUM ambapo katika jukwaa la viti vya Rangi Chungwa itakuwa Sh, 7,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000, na VIP A Sh 30,000.
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi Saa 2:00 asubuhi katika vituo vya Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).Aidha, amesema magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya Uwanja siku ya Jumapili.

No comments:

Post a Comment