Pages

Monday, April 21, 2014

SHIRIKISHO LA MCHEZO WA BAO LALAANI VIKALI WANASIASA KUWAKASHIFU WAASISI WA TAIFA LETU








Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania limelaani vikali wanasiasa wanao simama na kutoa maneno ya kejeli zidi ya waasisi wa Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani kwani huko ni kutokuwa na maadili yenye sura alisi ya Utanzania.



Hayo yamesemwa na Raisi wa shirikisho hilo Bw Monday Likwepa kwenye Mashindano ya Mchezo maalum wa Bao wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani yanayo fanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.



  "Shirikisho kwa kupitia mchezo huu na wadau wake wote wamesikitishwa na kukerwa sana na tunalaani vikali vitendo vya baadhi ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba na Wabunge wa Jamuuri ya Muungano kwa kutumia nafasi walizo pewa sasa wamegeuza na kuwatuhumu, zalilisha na kuwakashfu waasisi wa Muungano wetu Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume’’ Alisema Bw Likwepa.

No comments:

Post a Comment