Pages

Sunday, July 27, 2014

DIAMOND PLATNUMZ NA LADY JAYDEE WANG'ARA TUZO ZA AFRIMMA


Msanii wa Bongo fleva,Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.

Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’

Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.

Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.

Kwa mujibu wa africanmuzikmag.com Producer bora wa mwaka ni Dj Oskido wa South Africa aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda, Sheddy Clever wa Tanzania na Ogopa wa Kenya.

Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.

No comments:

Post a Comment