Pages

Thursday, July 24, 2014

MIZENGO PINDA KUWA MGENI RASMI KWENYE BARAZA LA EID


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Eid- ElL-Fitri.Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Suleiman Lolila baraza hilo litafanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa kumi kamili alasiri.Aidha taarifa hiyo imesema kuwa Sikukuu ya Eid-EL-Fitri inatarajiwa kuwa tarehe 28 au 29 julai 2014 kulingana na mwandamo wa mwezi.
Sikukuu hiyo itaadhimishwa kitaifa  katika Mkoa wa Dar es Salaam na swala itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa moja na nusu asubuhi.
Mufti na sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba anawatakia waislam wote na Wananchi kwa ujumla Eid-EL-Fitri njema

No comments:

Post a Comment