Pages

Monday, September 8, 2014

TAHADHARI!

Muonekano wa mojawapo ya link kutoka katika ujumbe wa email.
Hii ni tahadhali kwa watumiaji wa mitandao ya simu kuhusu utapeli ambao unaendelea kwa sasa ambapo kuna kundi la watu linatuma ujumbe mfupi kupitia simu za mkononi na barua pepe (email) zikiwataka watu kuhakiki akaunti zao. TAFADHALI USIFANYE HIVYO!
MOJAWAPO ya ujumbe kupitia barua pepe (email):
Ndugu customer,
Tusaidie kuweka akaunti yako salama.
Hivi karibuni, kumekuwa na kupanda kwa matukio ya usalama kwenye mtandao kuuliza wateja update huko Tigo pesa akaunti. Wakati tukiendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuweka mtandao wa Tigo pesa ya salama, Tunaomba watumiaji kutusaidia kuthibitisha akaunti zao na kuzifanya ziwe salama, tafadhali tembelea kiungo hiki kwa ajili ya uhakiki.
Regards, 
Tigo pesa66 Services ©



Ukitembelea link hiyo utakutana na sehemu inayokutaka kuweka namba ya simu na neno la siri.

No comments:

Post a Comment