GUY Scott (pichani) ambaye alikuwa makamu wa rais wa Zambia, amekuwa mtu mweupe wa kwanza kutawala nchi huru ya Afrika baada ya kupita kwa miaka mingi sasa.
Makamu huyo amecvhaguliwa kuongoza taifa la Zambia likisubiri uchaguzi mkuu baada ya kifo cha rais wake, Michael Sata kilichotokea usiku wa kuamkia leo mjini London, Uingereza.
Hata hivyo haijajulikana kama makamu huyo atakuwa na uwezo wa kugombea nafasi hiyo kwa kuwa yeye si kizazi cha tatu kwa mujibu wa katiba ya Zambia.
Uchaguzi mkuu wa kumpata rais wa Zambia unatakiwa kufanyika katika kipindi cha siku 90.
Taarifa ya mtu huyo mweupe kuwa kiongozi wa Zambia ilitoloewa na waziri wa Ulinzi Edgar Lungu ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Urais wakati Rais Sata ameenda kutibiwa nje.Amekufa akiwa na miaka 77 kw augonjwa ambao serikali ya Zambia haiusemi waziwazi.
Rais huyo alikuwa akitibiwa katika hospitali ya King Edward VII.
Scott alizaliwa 1944 kwa na ametoka kwa baba mhamiaji ambaye alikuwa daktari.
Akiwa ni mwanauchumi wa Cambridge alianza shughuli za siasa mwaka 1990 kwa kujiunga na MMD. Mwaka 1992 alichaguliwa kuwa waziri wa kilimo.
Alijiunga na chama cha Michael Sata cha Patriotic Front (PF) mwaka 2001 na baada ya ushindi wa Sata Septemba 2011 alichgaguliwa Makamu wa rais baada ya PF kupata ushindi katika uchaguzi ulikuwa na usnindani mkubwa.
Kifo cha rais huyo kimetokea siku chache baada ya taifa la Zam,bia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Waingereza.
Katibu wa baraza la mawaziri,Roland Msiska alisema kwamba mke wake Sata na mwanae walikuwa kandoni mwa kitanda wakati anafariki dunia.
Michael Sata amekuwa raisd wa pili kufa akiwa madarakani. Rais wa kwanza alikuwa Levy Mwanawasa mwaka 2008.

No comments:
Post a Comment