Mwanasheria wa Chama cha Chadema Tundu Lissu leo
ametangaza rasmi kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kaskazini baada ya uamuzi wa
mahakama juu ya kesi iliyokua imefunguliwa na Zitto Kabwe kuhusu kupinga
uanachama wake kujadiliwa.
Baada ya uamuzi huo millardayo.com pia imeongea na Tundu Lissu kupata uhakika
wa kinachosemekana na hizi ni sentensi zake>>’Tumemshinda,kesi yake imefutiliwa mbali amemabiwa atulipe
gharama na kwa vile ile kamali aliyocheza ya kupeleka kesi mahakamani
imeshindikana si mwanachama wetu tena sasa hii ni rasmi’Sentensi nyingine Tundu Lissu amesema>>’Katiba yetu inasema ukipeleka kesi kwenye mambo ya Chama kwenye mahakama unafukuzwa uanachama na kwa mujibu wa katiba si mwanachama wetu tena,hilo haliwezi kuwa kosa letu akamuulize jaji Mchome’.
Hata hivyo baada ya uamuzi huo Mwanasheria Alberto Msando ambaye ni Wakili wa Zitto Kabwe ameandika haya kwenye akaunti yake ya Instagram

Source: Millardayo.com


No comments:
Post a Comment