Pages

Monday, October 20, 2014

KAMATI YA MISS TANZANIA KUTOA MAELEZO KAMILI KESHO KUHUSU UTATA WA MISS TANZANIA

Alipotangazwa mshindi, Miss Tanzania 2014, Sitti, ambaye ni binti wa mbunge wa jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, alivikwa taji na mtangulizi wake Happyness Watimanywa, Miss Tanzania 2013.



Kufikia taji hilo la Miss Tanzania,2014 Bi Sitti ni mshindi wa mara ya ishirini tangu mashindano hayo yaanze tena nchini humo mwaka 1994. 



Kabla ya taji hilo, Bi Sitti alishinda mataji mawili likiwemo la Miss Chang'ombe na Miss Temeke yote ya mwaka 2014.



Pia ataiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World 2015.



Warembo 30 waliingia katika kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2014.



Wengi wanahoji umri halisi wa Bi Sitti Mtemvu wakisema alidanganya

Lillian Kamazima alikuwa mshindi wa pili, ambapo Jihhan Dimachk alishika nafasi ya tatu.



Mara baada ya kutwaa taji hilo kumeibuka utata juu ya umri wa Miss Tanzania 2014.



Habari zimezagaa katika mitandao ya kijamii, ambapo anatuhumiwa kudanganya umri wake. Kuna taarifa zinasema Bi Sitti alitaja kuwa ana umri wa miaka 18, jambo linalobishaniwa.



Lakini ukweli utajulikana Jumanne tarehe 21 Oktoba 2014, ambapo waandaji rasmi wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Lino International wameahidi kulitolea ufafanuzi suala hilo.

No comments:

Post a Comment