Pages

Wednesday, November 12, 2014

RAPPER MAARUFU GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA

Geez Mabovu
Geez Mabovu ni ambae hajavaa shati.
Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 12 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Geez Mabovu 2
Dennis ambae alikua mtu wa karibu wa Geez Mabovu amethibitisha pia kuhusu kifo cha Geez Mabovu na kusema rapper huyu aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya.
Kwa mujibu wa Denis, Geez atazikwa kesho jioni November 13 2014. #RIP

No comments:

Post a Comment