Pages

Showing posts with label Michezo kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Michezo kitaifa. Show all posts

Monday, November 3, 2014

KOCHA MSAIDIZI WA AZAM FC ABWAGA MANYANGA

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala ameachia ngazi. Ongala ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mwanamuziki .marehem Remmy Ongala amejiuzu kuifundisha timu hiyo yenye maskani yake Chamazi ambao ni mabingwa wa tetezi  kwa mujibu wa afisa habari wa timu hiyo Jaffar Idd akihojiwa na kipindi cha michezo cha redio one amekiri na kusema kocha huyo alikuwa  na mpango wa muda mrefu wa kutaka kwenda nje ya nchi kwa ajilin ya kusomea ukocha na ndiponalipoandika barua ya kuomba ruhusa ya kujiuzuri ili apate nafasi ya kwenda uingereza kuchukua mafunzo ya ukocha 
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, November 1, 2014

RAGE AKANUSHA KUIHUJUMU KLABU YA SIMBA

Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Ismail Aden Rage amekanusha tetesi kuwa amekuwa akiihujumu timu hiyo ili ifanye vibaya kwenye mechi zake. Kupitia Kikaangoni Live ya EATV, Rage alisema akiwa kama shabiki mkubwa wa Simba aliyoitumikia kwa muda mrefu, hawezi ili ipate matokeo mabovu.

“Kusema kweli siwezi kuihujumu timu yangu Simba nadhani mimi nimeitumikia kuliko watu wengine wengi tu hapa na pia hapa nilipofika kwa sasa Simba wana mchango wao mkubwa tu hivyo siwezi kuihujumu Simba,ila nachoweza kusema ni kwamba mashabiki pamoja na uongozi wa Simba uliopo madarakani sasa katika mpira kuna mambo matatu kushinda sare au kufungwa kwa hiyo tukubali haya matokeo,pia tuwape muda huenda timu ikabadilika mbele ya safari,” alisema. 
Hivi karibuni Simba iliwasimamisha wachezaji wake watatu, Shabani Kisiga, Amri Kiemba na Haruna Chanongo kutokana na kudaiwa kuchangia matokeo mabovu ya timu hiyo. 
Hata hivyo Rage alisema hafikirii kugombea nafasi yoyote kwenye klabu hiyo. “Sijafikiri kugombea nafasi ya Rais katika Klabu ya Simba kwani nahitaji kupumzika,sasa hivi uongozi wa simba ni mgumu sana,” alisema.
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, October 30, 2014

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA


TFF YAOMBA WADAU WABUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tzau uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.

SDL KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 22
Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyoketi jijini Dar es Salaam jana (Oktoba 29 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange ilipitia maandalizi maandalizi ya ligi hiyo ikiwemo mwongozo wake (roadmap).
Kwa mujibu wa mwongozo huo, usajili wa wachezaji utamalizika Oktoba 31 mwaka huu. Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Novemba 1 hadi 7 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajia kukutana Novemba 11 mwaka huu kwa ajili ya kupitisha usajili.
Pia Kamati ya Mashindano imepitisha viwanja vya timu zote, isipokuwa uwanja wa timu ya Mpanda United ya Katavi na ule wa Town Small Boys ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Uwanja wa Town Small Boys haukupitishwa kwa vile hauna uzio wa kudumu ( wa chuma) wa kutenganisha wachezaji na washabiki, na pia ufikaji wa timu Tunduru ni mgumu kutokana na ubovu wa barabara ikizingatiwa kuwa ligi hiyo itachezwa hadi kipindi cha Masika.
Kwa upande wa uwanja wa Mpanda United, umekataliwa kwa vile hauna vigezo vya msingi vinavyotakiwa ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo, kutokuwa na nyasi na uzio wa kudumu kutenganisha wachezaji na washabiki.
Kutokana na uamuzi huo, Mpanda United sasa itatumia Uwanja wa Mandela uliopo Sumbawanga wakati Town Small Boys itachezea mechi zake kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.

Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao kwenye mechi za ligi.
Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.
Lengo hasa la programu hiyo ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.
TFF ina imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika hoteli itakayotangazwa baadaye.
Wachezaji walioteuliwa ni Aishi manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).
Edward Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Hassan Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United), Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).
Aboubakary Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, October 25, 2014

TAZAMA STAND UNITED WALIVYOKUWA WAKIINGIA UWANJANI NA KATAPILA KUCHEZA NA YANGA

Stand United wakiingia uwanjani na katapila tayari kucheza na Yanga, mwenye shati la kitenge hapo mlagoni ni Mbunge wa Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini amekuwa bega kwa bega na timu ya Stand United.
SOMA ZAIDI >>> »

Sunday, October 19, 2014

VODACOM YATOA ZAWADI KWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigela(mwenye suti nyeusi)pamoja na Mchezaji bora wa Mwezi wa Septemba wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Anthony Matogolo wa timu ya Mbeya City(kushoto)wakionesha hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 1/= kwa mashabiki wa timu yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na  Mkuu wa wilaya hiyo kwa niaba ya wadhamini wakuu wa ligi kuu Vodacom Tanzania hapo jana kabla ya mechi kuanza baina ya timu Mbeya City na  Azam FC,Ambapo Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli moja bila na anaeshuhudia kulia ni Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFU) Seleman Harub.  
  Mchezaji bora wa Mwezi wa Septemba wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Anthony Matogolo wa timu ya Mbeya City akionesha kikombe chake.
 mtanange ukiendelea katika ligi kuu ya vodakom katika
uwanja wa sokoine
Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia goli lao lililofungwa na  Aggrey Morris katika mzunguko wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya timu hiyo na Mbeya City hapo jana/juzi Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli 1-0.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, October 18, 2014

SIMBA NA YANGA ZATOKA SARE YA 0 - 0 LEO UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

 
Nadir Haroub 'cannavaro' wa Yanga (kulia) akipambana na mshambuliaji wa Simba Elius Maguri(katikati).
 

 
Shabiki wa simba....
 
Mashabiki wa Yanga...
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, October 13, 2014

WAKILI DAMAS NDUMBARO AFUNGIWA KUJISHUGHULISHA NA SOKA KWA MIAKA SABA


Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha pesa. Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv.

Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.

Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu. Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa ‘ hadharani’ na vilabu huku vikisema kuwa ‘ havikumtuma’ kuzungumza yale ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa ‘ utashi’ wake mwenyewe, na si wao walimtuma.

‘ Kilichomuhuku’ ni yeye kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu. Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe

Chanzo:Michuzi blog
SOMA ZAIDI >>> »

Sunday, October 5, 2014

YANGA YAICHAPA JKT RUVU 2 - 1 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo.
Jaja akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.
Jaja akichuana na beki wa JKT RUVU, Madenge Ramadhani.
Jaja akichuana na beki wa JKT RUVU, Madenge Ramadhani.
Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.



 Edward Manyama akimtoka beki wa JKT Ruvu, Madenge Ramadhani.
 Kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
Mohamed Faki akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Kelvin Yondani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

Chanzo: Jiachie Blog.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, October 4, 2014

SIMBA SC BADO 'TIA MAJI TIA MAJI' LEO TENA YALAZIMISHWA SARE YA 1 -1 NA STAND UNITED

Kikosi cha Stand United.
Kikosi cha Simba.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri akishuhudia timu yake wakati ikicheza na Stand United.

Benchi la ufundi la Stand United.
Golikipa wa timu ya Stend United, John Mwenda akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe wakati wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka  Tanzania uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. (Picha na Francis Dande)   
John Mwenda akiwapanga wachezaji wake.
Mshambuliaji wa Simba, ibrahim Ajib akiwatoka mabeki wa Stand United.
kipa wa timu ya Stend United, John Mwenda akiukodolea macho mpira uliopigwa na Shaban Kisiga ukiingia wavuni wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliofanyika Uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli lao.
Wachezajhi wa Stande wakitoka mapumziko.

Wachezaji wa Stand United wakiwa katika =chumba cha waandishi wa habari wakati wa mapumziko badala ya kuingia katika chumba maalum kwa ajili ya timu hiyo.
Kocha wa stand United akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Mashabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakiwa vichwa chini.
Wakifuatilia mchezo huo uku wakiwa hawana matumaini ya ushindi..
Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe akimtoka beki wa Stand United, Idd Mobby.
Kocha wa Simba akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Okwi akitafuta mbinu za kumtoka Iddy Mobby wa Stand United.
Amis Tambwe akipiga kichwa katikati ya mabeki wa Stand United.
Elius Maguri akimtoka beki wa Stand United.
Elius Maguri akiambaa na mpira.
Maguri akiipangua ngome ya Stand United.
Idd Mobby akimdhibiti Emmanuel Okwi.
Beki wa Stand United akimbana Emmanuel Okwi.
Nawatoka hivi.........
Mwamuzi wa mchezo huo, Anthony Kayombo kutoka Rukwa akimuonyesha kadi ya njano John Mwenda.
CHANZO MICHUZI BLOG
SOMA ZAIDI >>> »