Pages

Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Friday, May 29, 2015

MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA AAPISHWA NA MKUU WA MKOA WA DODOMA LEO

Mhe. Athony Mavunde akila kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Hayupo Pichani) Mei 29,2015
Mhe. Athony Mavunde akitia saini hati ya kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa Mei 29, 2015
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto) akipongezwa na baba yake mzazi Ndg. Peter Mavunde mara baada ya kula kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya Mei 29,2015
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto kwake) na wajumbe wa kamatiya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma wakati wa Hafla ya kumuapisha Mkuu huyo mpya wa Wiaya ya Mpwapwa Mei 29,2015
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, April 25, 2015

MUUGUZI AMCHAPA VIBOKO MAMA MJAMZITO HADI KUSABABISHA KIFO CHA KICHANGA


Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani Dodoma, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.

Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya.

Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy. 
 
“Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.

Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika, alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.

“Kesho yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.

Alisema Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba 17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji.
 
 “Yaani ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.

Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo.

Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.
 
Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo.

Alisema pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito huyo.

“Mimi sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji, nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa kamili,” alisema.

Afisa Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, March 19, 2015

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI KUVISHA VYEO MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA WA DAR ES SALAM

unnamed
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(pichani) kesho tarehe 20 Machi, 2015 saa 8:00 mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria.
Kwa Mamlaka aliyopewa kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini atawavisha vyeo hivyo katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.Tume ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 2/2014/2015 kilichofanyika tarehe 16 Machi, 2015 chini ya Mwenyekiti Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb) imewapandisha vyeo
Maafisa 292 wa ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 16 Machi, 2015.Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza kuwa Kamishna Msaidizi wa Magereza 11, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza 41, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa Magereza 83 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza 157.
Imetolewa na; Inspekta Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
                       Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
                       DAR ES SALAAM
                       19 Machi, 2015.
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, March 13, 2015

RUFAA YA OSCAR PISTORIUS YATUPILIWA MBALI

 
Mwanariadha Oscar Pistorius.
 JAJI Thokozile Masipa ametupilia mbali rufaa ya mwanariadha anayehudumia kifungo cha miaka mitano jela kwa kumuua mpenzi wake, Oscar Pistorius huko Afrika Kusini.
 
Oscar Pistorius akiwa na Reeva Steenkamp.
 Rufaa hiyo iliwasilishwa na makili wa mwanariadha huyo ambaye ni mlemavu wa miguu.
Jaji Masipa ametoa uamuzi huo katika Mahakama ya Johannesburg nchini Afrika Kusini kwamba ombi hilo likataliwe.

Pistorius akiwa kazini.
 Pistorius alimpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp mwezi Februari 2013 na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kuua bila kukusudia.
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, February 18, 2015

BUNDUKI ILIYOPORWA TANGA YAKUTWA NA RISASI ZAKE 20

Bunduki iliyoporwa Tanga yapatikanaPOLISI mkoani Tanga imesema imefanikiwa kupata bunduki aina ya SMG, ikiwa na risasi 20 ndani ya mapango ya Majimoto katika eneo la Amboni, inayodaiwa ilikuwa ikitumiwa na wahalifu waliorushiana risasi na askari mwishoni mwa wiki.
Aidha, imesema inashikilia watu kadhaa akiwemo aliyesababisha kupatikana kwa bunduki hiyo. Baadhi ya watu wanaendelea kuhojiwa, kupata taarifa kwa lengo la kukamata waliopora silaha kwa askari na kurushiana risasi kwenye mapango hayo.
Kupatikana kwa silaha hiyo, kunafuatia msako maalumu uliodumu kwa siku nne sasa, uliolenga kusaka silaha na wahalifu wanaodaiwa kujificha ndani ya mapango ya mawe yaliyopo Amboni, nje kidogo ya mji wa Tanga.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema mafanikio hayo, yametokana na subira ya wakazi wa Tanga na ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuuonesha kwa Polisi inayoshirikiana na vikosi vingine vya ulinzi na usalama, kufanya operesheni ya pamoja kwenye eneo hilo.
“Kutokana na taarifa kutoka kwa wananchi Februari 16 mwaka huu katika kitongoji cha la ‘Kona Z’ kilichopo Amboni, tulifanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye kwa sasa sitamtaja jina kwa sababu upelelezi unaendelea, tulimhoji kwa kina akatupa taarifa kuhusu silaha hii,” alisema.
Alieleza, “Tulikwenda mpaka pangoni na kufanikiwa kupata SMG hii ikiwa na magazini moja na risasi 20… silaha hii ni miongoni mwa zilizoporwa kwa askari mwezi uliopita”.
Alisema licha ya kupatikana kwa silaha hiyo, watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo. Alisema upelelezi unaendelea kupata taarifa za kuwezesha kupatikana kwa silaha nyingine na vitu mbalimbali vilivyowahi kuibwa.
“Naomba wakazi wa Tanga na Watanzania kwa ujumla muendelee kuvuta subira na kutoa ushirikiano…endelezeni utulivu na mshikamano kwa jeshi la polisi, ili kwa pamoja tuweze kumaliza tatizo hili,” alisema.
Alisema upo umuhimu mkubwa kwa wananchi, kuendeleza utulivu kwa kutokubali kuamini taarifa potofu zenye kujenga hofu, zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kwa kuwa zinalenga kuwavuruga.
“Kimsingi jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama, linaamini na kuthamini kazi ya vyombo vya habari hasa vile makini, ambavyo vimeendelea kuwaarifu wananchi habari sahihi ambazo hazina ghilba wala kuwachanganya”, alisema.
Alikanusha taarifa zilizoenea mjini kwamba ipo miili ya wahalifu,iliyokutwa ndani ya mapango hayo, kutokana na mapigano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
“Ndugu zangu mwanzoni tulikuwa tukisikia harufu kali ya kama miili iliyooza, kweli tulijitahidi kutafuta na tukafanikiwa kuona mizoga ya ngedere na siyo binadamu ...wanyama hao walikuwa watatu na walikuwa na majeraha makubwa sana. Kwa hiyo hawakuwa watu, bali ni ngedere ndio walikokuwa wamekufa na kuoza humo pangoni,” alisema.
Akizungumzia mkakati wa kupata silaha iliyosalia na vifaa vingine vilivyoporwa, Chagonja alisema jeshi lake na kikosi cha operesheni hakitalala usingizi mpaka vitu vyote vipatikane.

SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, December 3, 2014

HITILAFU YA UMEME KWENYE LIFTI YASABABISHA TAFRANI BENKI YA NBC DAR

 Baadhi ya wafanyakazi wa  Benki ya NBC, wakivuka barabara kurejea tena ofisini baada ya kuzikimbia kutokana na hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye lifti ya dharula katika Makao Makuu ya benki hiyo, makutano ya mitaa ya Sokoine Drive na Azikiwe, Dar es Salaam leo. Hitilafu hiyo iliyotokea majira ya saa 3:30, ilisababisha tafrani kiasi cha wafanyakazi kuzikimbia ofisi kwenda Bustani ya Posta ya Zamani (picha ndogo).Wateja waliopatwa na zahama hiyo walielekezwa na uongozi kwenda kupata huduma kwenye matawi mengine ya benki hiyo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Wafanyakazi wakiwa kwenye bustani ya Posta ya Zamani iliyopo mbele ya jengo lao, baada ya kumbia tafrani hiyo

 Wafanyakazi wa Benki hiyo wakirejea ofisini baada ya kuhakikishiwa usalama majira ya saa 4;35 asubuhi
 Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wakiwa na vifaa vyao tayari kutoa huduma hiyo. Hata hivyo kwa mujibu wa Rukia Mtingwa alisema hakuna mfanyakazi wala mteja aliyeumia wakati wa tafrani hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa (katikati) akiwasilinana  na watu mbalimbali baada ya hali ya usalama kurejea
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (wa pili kulia) akizungmza na waandishi wa habari juu ya tafrani hiyo.
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, December 1, 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI JOSEPH NYUKI AKAMATWA NA POLISI MKOANI IRINGA

Akari  polisi  Iringa akimthibiti mwimbaji  wa nyimbo za injili mwinjilisti Joseph Nyuki maarufu kama balozi wa  Yesu  ambae  alikuwa akiuza  CD zake  mitaani  leo
Balozi  wa Yesu  akiendelea  kuthibitiwa na polisi
Askari  polisi  akimthibiti balozi wa Yesu
Balozi wa  Yesu  akithibitiwa wakati wa kampeni yake ya Injili Mtaa kwa Mtaa mjini Iringa  leo
Wananchi  Iringa  wakiwa  wamelizunguka gari  la Balozi wa Yesu  leo
Balozi  wa Yesu  akiwatuliza  wafuasi wake
Balozi wa Yesu  akienda  kupanda gari
Balozi  wa Yesu akiwa katika gari lake  tayari  kwenda Polisi  kutii  sheria bila Shuluti
Gari la  balozi wa Yesu  likiondoka kwenda  Polisi
Balozi  wa Yesu  akizungumza na mtandao   huu wa matukiodaima baada ya  kuachiwa na  polisi
Balozi  wa Yesu  akionyesha  CD  yake mpya ya Saluti ambayo alikuwa akiiuza  mtaani kabla ya  kuwapigia  saluti  polisi  waliomkamata kwa muda
Hii  ndio  CD  ya Saluti ambayo  leo balozi  wa Yesu  kajikuta  akiwapiga  kikweli kweli  Saluti  Polisi Iringa
MWIMBAJI  wa  nyimbo  za  injili maarufu nchini Tanzania ambae ni mlemavu  wa  mkono mmoja Mwinjilisi Joseph  Nyuki maarufu kwa jina la Balozi wa  Yesu ajikuta  mikonono  wa  polisi wakati akiendesha harambee yake ya Injili mtaa kwa Mtaa mjini Iringa.

Tukio  hilo la balozi  wa Yesu  kukamatwa na  polisi  limetokea  leo majira ya saa 8 mchana   wakati gari la mwimbaji huyo wa Injili likipita katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kueneza  injili kwa kuuza CD inayokwenda kwa  jina la Saluti .

Mbali ya  kuwa na  kibali  cha Manispaa ya  Iringa  kinachompa uhuru  wa kueneeza injili kwa watu  wote kupitia CD hiyo ya  Saluti na kibali  hicho  kupitishwa  polisi  bado  askari  polisi  walimfuata  balozi huyo wa Yesu  na kumtia nguvuni kuwa hapaswi  kueneza  injili  kwa  kupiga  kelele mitaani.

Askari  ambae  jina lake  halikuweza  kunaswa  mara moja  alifika katika gari  lenye namba  za Usajili T 364 DPD ambalo  lilikuwa   limefunga  muziki mnene  na kupeperusha  injili mtaani kiasi cha  kila mmoja  mjini hapa kuvutiwa na vionjo vya mwimbaji  huyo na  kulifuata  gari hilo  kununua CD kabla ya askari  huyo  kulipiga  pini gari   hilo eneo la  Soko  kuu Miyomboni mjini Iringa .

Baada ya  kumsimaisha mwimbaji huyo kutoendelea na uuzaji wa CD  hiyo askari  huyo alimtaka  kuonyesha kibali pamoja na kuzima  muziki na kugeuza  gari hilo kupeleka  Polisi amri  ambayo bila jeuri  balozi wa  Yesu  alitii huku akisema ndio kazi ya  kueneza  injili  hiyo ambayo kwake ameizoea .

Kwa  upande  wao  wananchi ambao  walikuwa  wakinunua CD  wameeleza  kusikitishwa na hatua ya  polisi  kuzuia  uenezaji wa injili huku  kila siku mji wa Iringa  watu  wanapita na magari  wakitangaza Ma Disco na matamasha  yenye vichocheo  vya maambukizi ya VVU huku  wakiyafumbia macho.

Mtandao   huu  ulipofuatilia  sakata   hilo  kituo  cha  polisi ulishuhudia suala  hilo  likiishia nje ya  kituo  cha polisi baada ya askari  huyo  kuyamaliza  kiume na mwimbaji huyo nje ya  kituo baada ya  kuonyesha kibali halali cha Manispaa ya Iringa na wakati  askari huyo akihoji  zaidi  juu ya kuzunguka  kila  kona likiwemo  eneo hilo la polisi kwa  kupiga muziki ghalfa Mungu alionyesha nguvu  zake  kufuatia gari  jingine  lililokuwa  likiuza  simu  huku  likipiga miziki ya duniani likipita nje ya  kituo cha  polisi  bila  kukamatwa  ndipo askari kwa kuona  hilo walimruhusu  kuendelea na kazi ya kuitangaza injili.

Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima  mara  baada ya  kuachiwa  huru Balozi wa Yesu  alisema   kuwa  polisi walifika  na kumsimamisha na kumwomba  kibali na baada ya  kuonyesha aliachiwa  huru na  kuwa  polisi  wametimiza  wajibu  wao na kuwa hana kinyongo nao.

Pia  alisema  kuwa ziara  yake  mkoani Iringa na mikoa mbali mbali ni kuitangaza  injili  kupitia oparesheni yake ya Injili mtaa  kwa Mtaa  kwa  watu  wote  waokoke  na kuwa anaifanya  hivyo kama  njia  ya kuuza CD  yake  baada ya  kuchoshwa na unyonyaji  unaofanywa na baadhi ya studio kwa kuwalalia  waimbaji wa nyimbo  za Injili nchini.

CHANZO:http://www.matukiodaima.co.tz/
SOMA ZAIDI >>> »

Tuesday, November 18, 2014

MOTO WATETEZA SOKO LA BIDHAA ZA UTAMADUNI LIITWALO MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET JIJINI ARUSHA


baadhi ya wakazi wakiangalia jinsi mali zilizotetekea na moto

baadhi ya wenye maduka wakiangalia baadhi ya mali zao zilizoungua

Baadhi mabaki ya maduka yakiendelea kuungua

baadhi wa wakazi wa arusha wakichakurachakura baada ya maduka yapatao 180 kuungua moto Arusha leo

watu mbalimbali wakiangalia baadhi ya mali za wafanya biashara 
SOMA ZAIDI >>> »