Pages

Showing posts with label Burudani kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Burudani kimataifa. Show all posts

Sunday, May 3, 2015

FLOYD MAYWEATHER AMCHAKAZA MANNY PACQUIAO


Najua watu wengi waliisubiri hii kwa hamu.. wengine hata sio mashabiki wa boxing lakini walijikuta wakivutiwa na hii.. Promo ilikuwa kubwa sana, pambano la kihistoria ambalo dunia nzima ililisubri ni hili kati ya Floyd ‘Money’ Mayweather na Manny Pacquiao.
Points tayari zimeamua, pambano limeenda kwa round 12, Floyd Mayweatherkamshinda Pacquiao kwa points za majaji watatu wote, 118 kwa 110, 116 kwa 112 na 116 kwa 112.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, October 25, 2014

SHAKIRA, JENIFFER LOPEZ WATUMIKA KWA UTANI WA EL CLASICO.

Ushabiki mkubwa wa klabu kubwa mbili za Hispania, Barcelona na Real Madrid, sasa umeingia kwenye sura nyingine.Mechi ya kesho ya El Clasico sasa imevushwa hadi kwa wanamuziki wawili nyota wanawake.Jennifer Lopez yeye ni Real Madrid wakati Shakira ni Barcelona.
Jennifer na Shakira ndiyo wamekuwa wakishindanishwa na mashabiki wao na kitendo cha kuwa timu tofauti kimefanya mashabiki wao kuingia kwenye ushindani pia.
Kila upande umekuwa ukitumia picha zao kuzungumzia mechi hiyo.
Katika mitandao ya kijamii, picha zao zimejaa lukuki.
Ushindani wa mechi hiyo, huwa mkubwa kuliko wa nyingine yoyote ya soka duniani.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, October 18, 2014

PICHA ZA T.I AKIWASILI TAYARI KWA SHOW YA FIESTA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 

 



SOMA ZAIDI >>> »

DAVIDO AZUIWA KUPIGA SHOW LEO FIESTA


Mahakama ya Kisutu yamzuia Davido kuperform katika tamasha la Fiesta*
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam imemzuia msanii kutoka
Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama 'Davido' kuperform katika tamasha la
Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na Prime Promotion, October 18,2014.
Amri hiyo imetolewa jana (October 17) na hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu mheshimiwa D. Kisoka kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa
mahakamani hapo na Times Fm Radio na Times Fm Promotion.

Times Fm Radio na Times Fm Promotion walipeleka maombi ya dharura
mahakamani hapo wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika
tamasha hilo kwa kuwa licha ya BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa
kutoa kibali cha msanii huyo kwa maelezo kuwa tayari alikuwa
ameshachukuliwa kibali cha kuperform nchini November 1 kwenye tamasha
lililoandaliwa na Times Fm Radio,  Clouds Fm na Prime Times Promotion
waliendelea na taratibu zote bila kujali zuio hilo la BASATA.

Times Fm Radio na Times Fm Promotion waliiomba mahakama kuidhinisha madai
yao dhidi ya Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni
inayomsimamia Davido, HKN Music.
Madai hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama na usumbufu
waliosababishiwa na walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama imetoa amri kuwa msanii huyo amezuiwa kufanya onesho hilo October
18,2014 hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana mhakamani hapo.
Awali, Davido alisikika katika matangazo ya Times Fm Radio akieleza kuwa
atakuja Tanzania November 1 kwa ajili ya kufanya onesho linaloandaliwa na
kituo hicho cha radio lililopewa jina la 'The Climax'.



SOURCE KILEO
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, October 17, 2014

MWANARIADHA PISTORIOUS BADO NI HALI TETE


Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius (kulia) akiwa na mpenzi wake, Reeva Steenkamp enzi za uhai wake.
Kesi ya mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius inaendelea leo siku ya nne mahakama kuu mjini
Pretoria, Afrika Kusini chini ya Jaji, Thokozile Masipa huku wakili wa Pistorious, Barry Roux akiendelea kujenga hoja kibao za kumtetea Pistorious.

Wakili wa Pistorious, Barry Roux akiongea jambo.
Wakili huyo ambaye amekuwa mtetezi tangu mwanzo wa kesi ya Pistorious, amekuwa akigoma kusikia hata kifungo cha nje endapo Pistorious atahukumiwa.

Jaji Judge Thokozile Masipa akiwa anasikiliza wakili wa Pistorius (hayupo pichani).
Ameendelea kusisitiza kuwa mahakama inabidi imuangalie Pistorious zaidi kimatibabu endapo atahukumiwa kwenda jela kwani anavyoamini gerezani hakuna matibabu mazuri kwa mgonjwa kama yeye.
Pistorius alipatikana na kosa la mauaji bila kukusudia mwezi jana na huenda akakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela, lakini jaji anaweza kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza tu faini.
GPL
SOMA ZAIDI >>> »

Tuesday, October 14, 2014

CHRIS BROWN AWAKERA MASHABIKI WAKE BAADA YA UJUMBE ALIOUANDIKA KWENYE TWITTER

Christopher Maurice "Chris" Brown.
MWIMBAJI mashuhuri duniani, Christopher Maurice "Chris" Brown ameonekana kuwakera mashabiki wake baada ya jana kutuma ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter kuhusu Homa ya Ebola na kutoa maoni yake.
Maoni aliyoandika Chris Brown.
Brown alindika hivi: ''Sijui, lakini nadhani janga la Ebola ni njia mojawapo ya kupunguza idadi ya watu duniani, janga hili linatisha kweli,''.
Ujumbe huo ulionekana kuwakera sana mashabiki wake ambapo baadhi walimjibu kuwa kama hana cha kusema bora akakaa kimya.
Muda mfupi baada ya staa huyo kubaini kuwa ujumbe wake huo umewakera watu aliandika hivi: ''Afadhali niwe kimya".
Homa ya Ebola mpaka sasa imesababisha vifo vya zaidi ya watu 4,000 katika ukanda wa Afrika Magharibi.

SOMA ZAIDI >>> »

Friday, October 3, 2014

DIAMOND PLATNUMZ APONGEZWA NA BASATA KWA KUSHINDA TUZO YA MTV

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo ya Msanii bora wa mwezi wa kituo cha televisheni cha MTV Base kinachorusha matangazo yake kutoka Afrika Kusini na kuyafikia maeneo mengi duniani.

Aidha, Baraza linampongeza msanii huyu na wenzake Peter Msechu na Vannessa Mdee kwa kuchaguliwa kushindania tuzo mbalimbali katika tuzo za “All Africa Music” (Afrima) ambapo nyimbo zaidi ya 2025 kutoka kwa wasanii mbalimbali barani Afrika zinatarajiwa kushindanishwa na washindi kupatikana.

Kuteuliwa na kushinda kwa Wasanii wa Tanzania katika tuzo mbalimbali za Afrika na duniani ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na nje ya Tanzania.

Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kulitangaza na kukuza soko la kazi zao kimataifa.

Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za kutambuliwa na Serikali.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, October 1, 2014

DIAMOND PLATNUMZ TENA AIBUKIA KWENYE TUZO ZA NCHINI NIGERIA


Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo nyingine za kimataifa zinazofahamika kama ‘THE HEADIES 2014’, ambazo ni tuzo kubwa nchini Nigeria. 
Nasib Abdul ametajwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Afrika (Best African Arstist) ambacho kinawaniwa na wasanii wa nje ya Nigeria. Katika kipengele hicho anashindana na Mafikizolo, Sarkodie na R2Bees.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika October 25, 2014. 
Wasanii wengine wa Nigeria waliotajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele tofauti ni pamoja na Davido, Wizkid, 2Face, Tiwa Savage, KCee, Burna Boy na wengine. 
Kuhusu Tuzo za THE HEADIES 
Also referred to as Hip Hop world awards; The Headies since debuting in 2006 has become one of the most anticipated events year in year out. Today, the Awards ceremony is the biggest award ceremony in the country. Within the space of six years it has cemented itself as the authentic awards’ brand and has continued to deliver an annual awards ceremony that has never failed to dazzle, inspire, excite and entertain. In Nigeria’s entertainment calendar, the date for the Hip Hop World Awards is one of the most anticipated, if not the most important.
Conceived to reward artistes with genuine artistic talent in a developing music industry, The Headies debuted on March 10, 2006 at the MUSON Centre Onikan, Lagos. Tagged “The revolution is here”, the event was hosted by Darey Art Alade and left many spell bound and dazzled by the sheer brilliance and glamour of the event. It was the first time that an awards ceremony of international standard was organized in its entirety by Nigerians.
Everything about the awards was a first; from the limousine rides, the red carpet, the stage to the well choreographed and rehearsed performances.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, April 19, 2014

MADAKTARI WASHINDWA KUUNGANISHA UUME WA MWANAMUZIKI ALIYE JIKATA MAKUSUDI



Rapper mwenye uhusiano na kundi la Wu-Tang Clan, Andre Johnson hana tena kiungo kinachomfanya aitwe mwanaume kwakuwa madaktari wameshindwa kuunganisha.


Mtandao wa TMZ uliandika kuwa Johnson aka Christ Bearer aliukata uume wake jana Jumatano na kujirusha kwenye nyumba ya ghorofa mbili anakoishi huko North Hollywood kwa kile kinachodaiwa kutaka kujiua. Alikimbizwa kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center lakini uume wako umedaiwa kukatika kabisa.

Johnson/Christ Bearer ni member wa kundi liitwalo Northstar, lilioanzishwa na rapper Wu-Tang Clan, RZA. Kulikuwepo na rappers wengine kwenye tukio hilo waliokanusha kuwepo na madawa ya kulevya kiasi cha kumfanya achukue uamuzi huo. Wanaamini kuwa Johnson/Christ Bearer anaweza kuwa na matatizo ya kiakili.
SOMA ZAIDI >>> »