Pages

Showing posts with label kimataifa. Show all posts
Showing posts with label kimataifa. Show all posts

Friday, October 24, 2014

PRESIDENT KIKWETE AWARDED HONORARY PROFFESSORSHIP BY CHINA AGRICULTURAL UNIVERSITY


President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete being awarded Honorary Professorship at the China Agricultural University in Beijing this evening. On the left is Chair of the University Council Jiang Peimin and on the right is the University’s President Professor KE Bingsheng.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech shortly after he was awarded Honorary Professorship at the China Agricultural University in Beijing this evening. President Kikwete is in China for a working visit at the invitation of the China President Xi Jinping(photos by Freddy Maro).
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete tour the greenhouse shortly after he arrived at China Agricultural University this afternoon. President Kikwete later addressed the University students and lecturers on the agricultural development in Tanzania before being conferred Honorary Professorship.
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, July 18, 2014

PICHA MBALI MBALI ZA AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA BAADA YA KULIPULIWA JANA HUKO MASHARIKI MWA UKRAINE

Ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777-200 ikiteketea kwa moto baada ya kulipuliwa.
Mmoja wa waasi wanaoiunga mkono Urusi akiwa eneo la ndege iliyolipuliwa.
Waokoaji wakikagua katika mabaki ya ndege hiyo.
Baadhi ya miili ya watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo iliyolipuliwa na kuanguka kijiji cha Grabovo kilichopo maili 30 kutoka mpaka wa Urusi na Ukraine.
Wananchi wakiweka maua katika eneo lililoandaliwa nje ya ubalozi wa Uholanzi huko Kiev, Ukraine.
Baadhi ya mizigo ya abiria waliokuwa ndani ya ndege iliyolipuliwa.
Vikosi vya zimamoto vikipambana na moto uliokuwa ukiteketeza ndege ya Malaysia.
Waasi wanne wa Ukraine wanaoiunga mkono Urusi wakiwa eneo la ajali. Waasi hao ndiyo wanaodaiwa kuilipua ndege hiyo.
MAMLAKA nchini Uholanzi imesema kuwa watu 154 raia wa Uholanzi, 27 wa Australia na tisa wa Uingereza walikuwa miongoni mwa watu 298 waliopoteza maisha katika ndege ya shirika la Malaysia aina ya Boeing 777-200 yenye namba MH17 iliyolipuliwa mashariki mwa Ukraine jana.
Maafisa nchini Ukraine wamesema ndege hiyo ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kuelekea Kualar Lumpur ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo kwenye kijiji cha Grabovo kilichopo maili 30 kutoka mpaka wa Urusi na Ukraine ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amelitaja tukio hilo kama kitendo cha ugaidi huku Rais wa Urusi Vladimir Putin akiishutumu Ukraine kwa kutodumisha amani nchini mwake.
Maafisa wa Ukraine walichapisha kile walichotaja kuwa mawasiliano ya simu yaliyonaswa kati ya waasi wakiwaeleza maafisa wa Urusi kwamba ni wao ndio waliohusika katika kuindungua ndege hiyo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ukraine, Pavlo Klimkin, amesema kuwa serikali ina ushahidi wa kutosha kwamba ndege hiyo ilidunguliwa.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miezi minne tangu ndege nyingine ya shirika hilo la Malaysia kupotelewa ndege aina ya Boeing 777-200ER iliyokuwa na namba MH370 ikiwa na watu 239 kutoka mataifa 14 ambayo mpaka sasa bado haijulikani ilipo.
SOMA ZAIDI >>> »

Sunday, June 29, 2014

WATU ZAIDI YA 130 WAMENASA KWENYE KIFUSI CHA JENGO LILILOPOROMOKA NCHINI INDIA


Jengo la makazi laporomoka Mumbai, India

Maafisa nchini India wamesema wanahofu kuwa zaidi ya watu 130 wamenasa kwenye kifusi cha jengo lililoporomoka kusini mwa India,takriban Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha katika tukio hilo mjini Porur.wengi wa walionasa wanaaminika kuwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga jengo la ghorofa 11.

Kikosi ha uokoaji kinafanya jitihada za kuokoa walioathiriwa na ajali hiyo. siku ya jumamosi, watu 10 ,miongoni mwao watoto watano, walipoteza maisha mjini Delhi,baada ya jengo la makazi ya watu kuporomoka.

India imekua ikikumbwa na matukio ya kuporomoka kwa majengo, sababu ikielezwa kuwa usalama usio madhubuti na ujenzi usiozingatia viwango bora.

Mwezi Januari mwaka huu, takriban watu 14 walipoteza maisha baada ya jengo lililokuwa kwenye hatua za ujenzi kuporomoka katika jimbo la Goa.

Takriban watu 42 walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na Jengo la ghorofa nne mjini Mumbai mwezi Septemba mwaka jana.

Chanzo ; BBC Swahili
SOMA ZAIDI >>> »

UJUMBE WA RAIS OBAMA KWENYE MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

On behalf of the American people, Michelle and I extend our best wishes to Muslim communities here in the United States and around the world on the beginning of the blessed month of Ramadan.A time for self-reflection and devotion through prayer and fasting, Ramadan is also an occasion when Muslims around the world reaffirm their commitment to helping the less fortunate, including those struggling because of economic hardship and inequality.  Here in the United States, we are grateful to the many Muslim American organizations, individuals, and businesses that are devoted to creating opportunity for all by working to reduce income inequality and poverty, not only through their charitable efforts, but also through their initiatives to empower students, workers and families with the education, skills and health care they deserve.

Ramadan also reminds us of our shared responsibility to treat others as we wish to be treated ourselves and the basic principles that bind people of different faiths together:  a yearning for peace, justice, and equality.  At a moment when too many people around the world continue to suffer from senseless conflict and violence, this sacred time reminds us of our common obligations to pursue justice and peace and to uphold the dignity of every human being. 
As I’ve done every year as President, I look forward to welcoming Muslim Americans from across the United States to the White House for an iftar dinner.  It will be another opportunity for me to convey America’s appreciation for the contributions of Muslim Americans to our country and to wish Muslims around the world a month blessed with the joys of family, community, peace and understanding.  Ramadan Kareem
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, May 19, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. GHARIB BILAL KATIKA ZIARA YA KIKAZI NCHINI JAPAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Biashara, Uchumi na Viwanda wa Japan, Toshimitsu Motegi, (wa kwanza kulia) wakati alipofika ofisini kwa Waziri huyo kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo Mei 19, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona. 



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana zawadi na Waziri wa Biashara, Uchumi na Viwanda wa Japan, Toshimitsu Motegi, baada ya mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo Mei 19, 2014.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya JETRO, Hiroyuki Ishige, wakati walipokutana na kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana zawadi na Mwenyekiti wa Kampuni ya JETRO, Hiroyuki Ishige, baada ya mazungumzo yao wakati Makamu Dkt Bilal, akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa JAICA, Akihiko Tanaka, yaliyofanyika wakati walipokutana kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake nchini Japan, leo Mei  19, 2014. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa JAICA, Akihiko Tanaka, yaliyofanyika wakati walipokutana kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake yake leo
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, May 3, 2014

WATU 2000 WAFUKIWA KWA UDONGO HUKO NCHINI AFGHANISTAN



Udongo ulioporomoka na kufunika baadhi ya nyumba

Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa wa karibu mita kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Miili ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana makazi.

Baadhi ya watu wakiangalia kama wapo walio hai 


Eneo kubwa limefunikwa na udongo

Mashirika ya misaada na uokoaji kwa sasa wameanza kuwapa mikate na maji maelfu ya watu waliolala nje kwenye baridi kali wakiwa hawana makazi.
"Taarifa zinasema ardhi na matope yameendelea kuporomoka ambapo wengi ya waliokufa ni waokoaji ambao walikwenda kutoa msaada kwa wenzao."
Kuna taarifa nyingine zinazosema maelfu mengine ya watu huenda wakawa wametoweka baada ya upande mmoja wa mlima kuangukia kijiji k katika eneo la mashambani la mkoa wa Badakhshan unaopakana na mataifa ya Tajikistan,Uchina na pakistan.
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo.
SOMA ZAIDI >>> »

WAANGALIZI WA KIMATAIFA WA OSCE WAACHIWA HURU NCHINI UKRAINE


Waangalizi wa kimataifa OSCE waliokuwa wakishikiliwa Ukraine

Waangalizi 7 wa kimataifa waliokamatwa siku nane zilizopita na wanaharakati wanaounga mkono Urusi,wamewachiliwa huru,pamoja raia watano wa Ukraine waliokuwa nao.
Kiongozi wa kundi la raia wa Ukraine wanaotaka kujitenga na taifa hilo mjini Sloviansk Vyacheslav Ponomaryov ,ameelezea kwamba waangalizi hao ni wageni wake na kwamba wamewachiliwa bila vikwazo.
Urusi imekuwa chini ya shinikizo ya mataifa ya magharibi kuwaachilia huru waangalizi hao ili kupunguza hali ya wasiwasi mashariki mwa Ukraine.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo amesema kuwa waangalizi hao waliweza kuachiliwa huru kupitia mjumbe mmoja wa Urusi Vladmir Lukin.
SOMA ZAIDI >>> »

Tuesday, April 29, 2014

MAKOMBORA YAVURUMISHWA MJI MKUU WA SYRIA,DAMASCUS



Maelfu wa wakimbizi wa Syria wanakumbwa na hali ngumu huku vita vikiendelea

Msururu wa makombora yamevurumizwa katikati mwa mji wa Damascus, na kuwauwa watu 12 huku hamsini wakijeruhiwa.
Shirika la habari la Syria limesema kituo kimoja cha ufundi na hata shule zimeshambuliwa .
Kadhalika shirika hilo limesema waasi ndio waliofanya shambulio hilo.
Serikali imekuwa ikishambulia maeneo yanayokaliwa na waasi karibu usiku na mchana.
Shambulizi hili linakuja siku moja baada ya rais Bashar Assad kusema atasimama kugombea tena uongozi wa nchi hiyo akiipuuza wito wa jamii ya kimataifa kuwa ajiondoe madarakani ili kutafuta suluhu la vita vya syria.
Wanajeshi wamewaondoa wapiganaji kutoka maeneo mengi waliyokuwa wanadhibiti na yanayozingira mji mkuu Damacus, lakini wakazi wanasema wapiganaji hao wamezidisha mashambulizi ya roketi na makombora mjini Damascus.


                        Rais Assad anatarajiwa kushiriki uchaguzi mkuu unaokuja

Neno magaidi linatumiwa na maafisa wakuu wa Syria, kuwalenga wale wanaopigana kuiangusha serikali ya Rais Assad.
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria linasema kuwa idadi ya majeruhi katika vita hivyo huenda ikaongezeka.
Zaidi ya watu 150,000 wameuawa katika vita hivyo vilivyodumu miaka mitatu sasa.
Mamilioni ya wengine wamelazimika kutoroka makwao huku mapigano yakiendelea kutokota.
Wengine zaidi ya milioni tatu na nusu wanaosa msaada muhimu ikiwemo dawa na chakula.
SOMA ZAIDI >>> »

MAREKANI YATOA VIKWAZO VIPYA VYA KIUCHUMI DHIDI YA URUSI





Marekani imetoa taarifa kuhusu vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi na kuushutumu utawala wa Moscow kwa kushindwa kutimiza mkataba wa kimataifa uliolenga kusuluhisha mzozo wa Ukraine.
Vikwazo hivyo vimelenga washirika wa Karibu wa Rais wa Urusi Vladmir Putin na vimeongeza orodha ya vikwazo vilivyowekwa hapo awali kwa baadhi ya maafisa wa nchi hiyo baada ya Moscow kutwaa eneo la Crimea mwezi uliopita.
Miongoni mwa waliolengwa ni mmoja wa wanasiasa maarufu nchini Urusi Igor Sechinambaye wakati mmoja alikuwa afisa wa ujasusi na sasa ni afisa mkuu katika kampuni ya mafuta ya Rosneft ambayo kwa kiwango kikubwa inadhibitiwa na serikali.
Karibu asilimia sitini ya kampuni hiyo inamilikiwa na kampuni ya mafuta ya uingeza BP na thamani ya hisa za kampuni hiyo ilishuka punde tu baada ya taarifa kuhusu vikwazo hivyo kutolewa.
Wengine waliolengwa ni Alexei Pushkov, ambaye huongoza kamati ya mambo ya nje katika bunge la Urusi,Naibu waziri mkuu na kampuni kumi na saba za Urusi.
Akizungumza hapo awali Rais Putin alisisitiza kuwa Ukraine haitaathirika kiuchumi kutokana na vikwazo hivyo.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema nia ya Marekani sio kumlenga moja kwa Rais Putin lakini ni katika juhudi za kuishawishi Urusi kufuata mwelekeo unaofaa.
Muungano wa Ulaya pia umetangaza vikwazo vya usafiri na kuzuiliwa kwa mali dhidi ya watu 15 nchini Urusi lakini majina yao bado hayajatajwa.
SOMA ZAIDI >>> »

Tuesday, April 22, 2014

MTALII MUINGEREZA AZUIWA KUINGIA SRI LANKA BAADA YA KUBAINIKA AMECHORA 'TATOO' YA PICHA YA BUDHAA


Tatoo ya Naomi Michelle Coleman inaonyesha picha ya Budhaa ambaye ni Mungu waumini wa dini ya Budhaa. 
Mtalii mmoja muingereza amekataliwa kuingia nchini Sri Lanka baada ya kupatikana akiwa amechorwa 'Tattoo' ya Budhaa kwenye mkono wake.
Naomi Michelle Coleman, alikamatwa na maafisa wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada ya maafisa wakuu kuiona 'Tattoo' hiyo kwenye mkono wake wa kulia.
Budhaa alikuwa mtu mwenye busara na hekima kubwa na pia mwanzilishi wa dini hiyo ambayo mafunzo yake mengi yalijenga msingi wa dini yenyewe.
Msemaji wa polisi alisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini.
Hakimu aliamuru Bi Coleman arejeshwe nchini mwao.
Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao.
Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.
Bi Coleman aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bandaranaike siku ya Jumatatu kutoka nchini India ambapo maafisa punde ya kuiona Tattoo hiyo ya Budhaa akiwa amekaa kwenye mauwa, walimkamata.
Mwezi Machi mtalii mwingine muingereza, alizuiwa kuingia katika uwanja huo baada ya maafisa kusema kuwa alijibu kijeuri alipohojiwa kuhusu Tattoo aliyokuwa amechorwa ambayo pia ilikuwa na Budhaa.

Bi Coleman anazuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao 


Maafisa wa Sri Lanka ni wakali sana kwa watu wanaoonekana kudhihaki dini ya Budha
SOMA ZAIDI >>> »