Pages

Showing posts with label Chadema. Show all posts
Showing posts with label Chadema. Show all posts

Friday, March 13, 2015

POLISI KUCHUNGUZA KUHUSIANA NA MADAI YA DOKTA WILBROAD SLAA


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeanza kuchunguza malalamiko ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa ya kutaka kulishwa sumu na Mlinzi wake.

Madai hayo ambayo yamekuwa gumzo katika vyombo vya habari wiki hii huku wananchi wakihoji uhalisia wake, yamemuhusisha mlinzi huyo wa Dk Slaa huku yeye mwenyewe akikataa tuhuma hizo na kudai kuwa ameteswa na walinzi wa chadema.

Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova  amesema hayo  leo alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu taarifa hizo zilizofikishwa katika kituo cha polisi cha Oysterbey kupitia wakili wa Chadema John Malya ambae aliambatana  na  mtuhumiwa Khalid Kagenzi (48) ambaye ni mlinzi wa Dk. Slaa ili akatoe maelezo kwa niaba yake.

Mlinzi wa Dk. Slaa alidai kuwa ana majeraha mwilini yaliyotokana na mateso aliyofanyiwa akiwa chini ya ulinzi mkali  wa maafisa wa usalama wa Chadema ambao walikaa naye na kumhoji kuanzia tarehe 07/03 saa tano asubuhi hadi tarehe 08/03 mwaka huu saa kumi jioni.

Aidha Kamanda Kova amesema kuna mambo mawili yanafanyiwa uchunguzi likiwemo la mlinzi Khalid Kagenzi  na la pili ni dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa kumtesa kwa kumshambulia  mlinzi huyo  na kumsababishia majeraha mwilini mwake.

Kova aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili ni  Boniface Jacob, (32) mkazi wa kisiwani Ubungo, ambae ni diwani kata ya Ubungo kupitia Chadema,Hemed Ally Sabula (48) mkazi wa Tandale kwa Tumbo ambae Afisa Usalama wa Chadema,Benson Mramba (30)mkazi wa Tabata Kisukuru ,Afisa Utawala wa Chadema.

Aliongeza kuwa watuhumiwa hao watatu wapo chini ya ulinzi kwa makosa yaliyotajwa dhidi ya Khalid Kagenzi  na shauri litafikishwa mahakamani  kupitia kwa wakili wa serikali ili kujiridhisha  kisheria  na hatimaye kutoa maamuzi kuhusu mashtaka yao.
SOMA ZAIDI >>> »

Tuesday, March 10, 2015

CHADEMA YAMVUA RASMI UANACHAMA ZITTO KABWE

tundu lissu pc 
Mwanasheria wa Chama cha Chadema Tundu Lissu leo ametangaza rasmi kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kaskazini baada ya uamuzi wa mahakama juu ya kesi iliyokua imefunguliwa na Zitto Kabwe kuhusu kupinga uanachama wake kujadiliwa.
Baada ya uamuzi huo millardayo.com pia imeongea na Tundu Lissu kupata uhakika wa kinachosemekana na hizi ni sentensi zake>>’Tumemshinda,kesi yake imefutiliwa mbali amemabiwa atulipe gharama na kwa vile ile kamali aliyocheza ya kupeleka kesi mahakamani imeshindikana si mwanachama wetu tena sasa hii ni rasmi’
Sentensi nyingine Tundu Lissu amesema>>’Katiba yetu inasema ukipeleka kesi kwenye mambo ya Chama kwenye mahakama unafukuzwa uanachama na kwa mujibu wa katiba si mwanachama wetu tena,hilo haliwezi kuwa kosa letu akamuulize jaji Mchome’.
Hata hivyo baada ya uamuzi huo Mwanasheria Alberto Msando ambaye ni Wakili wa Zitto Kabwe ameandika haya kwenye akaunti yake ya Instagram
msandooo2
msandooo

Source: Millardayo.com
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, November 14, 2014

MBOWE AMESEMA HANA UGOMVI NA ZITTO KABWE

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hana ugomvi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa kuwa amemlea na amemesaidia vitu vingi zikiwamo fedha, gari, kula na kulala nyumbani kwake.Mbowe alisema Chadema hakijamtenga Zitto bali alijitenga mwenyewe na kufafanua kuwa Chama hicho hakiwezi kujengwa na viongozi ambao ni wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyasema hayo jana katika Kata ya Kalinzi, Jimbo la Kigoma Kaskazini katika ziara zake za ‘operesheni delete CCM’ kuelimisha wananchi kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa Katiba iliyopendekezwa.
Mbowe alisema hayo baada ya kuruhusu maswali kutoka kwa wananchi ndipo Cheche wa Cheche alipomuuliza kwamba kwa nini Zitto hayumo katika ziara hiyo wala ya Katibu Mkuu, Dk.Willibrod Slaa
“una baadhi ya watu wanafikiri kuwa nampiga vita Zitto, siwezi kumpiga vita Zitto kwa kuwa nimemlea, amekula na kulala nyumbani kwangu nami ndie nilimshauri kugombea ubunge na kumpa fedha pamoja na gari, iweje leo nimpige vita?” alihoji Mbowe wakati akijibu swali hilo.
SOMA ZAIDI >>> »