Pages

Showing posts with label Afrika. Show all posts
Showing posts with label Afrika. Show all posts

Monday, June 1, 2015

PICHA YA MKE WA RAIS MPYA WA NIGERIA AKIWA NA MABINTI ZAKE

 
Mke wa Rais wa Nigeria, Mrs Buhari akiwa na mabinti zake 
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, October 29, 2014

GUY SCOTT: RAIS WA KWANZA MWEUPE KUITAWALA ZAMBIA BAADA YA KIFO CHA RAIS MICHAEL SATA


GUY Scott (pichani) ambaye alikuwa makamu wa rais wa Zambia, amekuwa mtu mweupe wa kwanza kutawala nchi huru ya Afrika baada ya kupita kwa miaka mingi sasa.
Makamu huyo amecvhaguliwa kuongoza taifa la Zambia likisubiri uchaguzi mkuu baada ya kifo cha rais wake, Michael Sata kilichotokea usiku wa kuamkia leo mjini London, Uingereza.
Hata hivyo haijajulikana kama makamu huyo atakuwa na uwezo wa kugombea nafasi hiyo kwa kuwa yeye si kizazi cha tatu kwa mujibu wa  katiba ya Zambia.
Uchaguzi mkuu wa kumpata rais wa Zambia unatakiwa kufanyika katika kipindi cha siku 90.
Taarifa ya mtu huyo mweupe kuwa kiongozi wa Zambia ilitoloewa na  waziri wa Ulinzi Edgar Lungu ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Urais wakati Rais Sata ameenda kutibiwa nje.Amekufa akiwa na miaka 77 kw augonjwa ambao serikali ya Zambia haiusemi waziwazi.
Rais huyo alikuwa akitibiwa katika hospitali ya King Edward VII.
Scott alizaliwa 1944 kwa  na ametoka kwa baba mhamiaji ambaye alikuwa daktari.
Akiwa ni mwanauchumi wa Cambridge alianza shughuli za siasa mwaka 1990 kwa kujiunga na MMD. Mwaka 1992 alichaguliwa kuwa waziri wa kilimo.
Alijiunga na chama cha Michael Sata cha Patriotic Front (PF) mwaka 2001 na baada ya ushindi wa Sata Septemba 2011 alichgaguliwa Makamu wa rais baada ya PF kupata ushindi katika uchaguzi ulikuwa na usnindani mkubwa.
Kifo cha rais huyo kimetokea siku chache baada ya taifa la Zam,bia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Waingereza.
Katibu wa baraza la mawaziri,Roland Msiska alisema kwamba mke wake Sata na mwanae walikuwa kandoni mwa kitanda wakati anafariki dunia.
Michael Sata amekuwa raisd wa pili kufa akiwa madarakani. Rais wa kwanza alikuwa Levy Mwanawasa mwaka 2008. 
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, October 27, 2014

NAHODHA WA TIMU YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

 
Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi. Jeshi la polisi la nchi hiyo limesema.Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.
Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.
Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.
SOMA ZAIDI >>> »

Tuesday, October 21, 2014

PISTORIOUS AHUKUMIWA MIAKA 5 JELA

Mahakama ya Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miaka 5 jela mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. 

Mwezi September, mahakama hiyo ilimkuta Pistorius na hatia ya kumuua Reeva Steenkamp bila kukusudia katika siku ya wapendanao mwaka jana (February 14,2013). 
Pistorius alikiri kumpiga risasi Reeva nyumbani kwake na kujitetea kuwa alidhani ni mtu aliyevamia nyumbani kwao usiku ule. 
Akitoa masharti ya hukumu hiyo, jaji ameeleza kuwa Pistorius anapaswa kutumikia angalau 1/6 (Miezi 10) ya adhabu yake kabla hajafikiriwa kwa lolote.
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, October 17, 2014

BOKO HARAM MBIONI KUWAACHIA HURU WASICHANA 200 WALIOWATEKA

Boko Haram
Serikali ya Nigeria imesema wamefikia makubaliano ya kusitisha mapambano na kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram, ambapo katika taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na makubaliano hayo imesema kuwa wameafikiana kuhusu kuachiliwa huru kwa wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara huko Chibok.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa serikali ya Nigeria, Hassan Tukur amesema maafikiano hayo yamefikiwa leo baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya upande wa serikali na wawakilishi wa kikundi hicho, yaliyodumu kwa takribani mwezi mmoja.
Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na yale yaliyofanywa mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais wa Chad, Idris Derby.
Tukur amesema kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, japo muafaka zaidi juu ya hilo utapatikana punde baada ya kumalizika mkutano mwingine unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini Chad.
Bado haijafahamika kama makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili yanahusisha na matakwa yaliyotolewa awali na kundi la Boko Haram kutaka kubadilishana wasichana hao na wafungwa ambao ni wapiganaji wa kikundi hicho wanaoshikiliwa na serikali ya Nigeria.
SOMA ZAIDI >>> »

Sunday, October 5, 2014

GENERETA YAUA FAMILIA NZIMA



Mwili wa mama, na wa mmoja wa watoto unaonekana kwa mbali nyuma yakeMume, mke na watoto wao watatu wamefariki dunia baada ya kupumua hewa iliyojaa gesi ya “carbon monoxide” iliyokuwa ikitolewa na generator waliloliwasha ndani ya nyumba yao .
  

Katika dhahama hiyo iliyotokea Lagos, Nigeria, miili ya wahanga wote watano iligunduliwa na majirani zao. Majirani wameripoti kuwa baba wa familia hiyo alinunua generator siku mbili kabla ya kukutwa na umauti, na kuliweka chumbani kwake akihofia kuwa litaibwa akiliweka nje.


Siku iliyofuatia, majirani waligundua kuwa wanafamilia hao wote walikuwa kimya, na ndani ya nyumba yao siku nzima, hivyo mmoja wao akaamua kuangalia kujua kinachoendelea. Jirani huyo aliona miili ya marehemu, na kuwataarifu wenzake. Walipoingia ndani ya nyumba, walistushwa na janga walilokutana nalo.
Katika moshi unaotolewa na majenereta, kama wa mkaa, magari, pikipiki, na mashine nyingi, kuna gesi ya “carbon monoxide (CO)” ambayo, ni sumu inayokusababisha kuchoka, kupoteza fahamu, na hatimaye kufariki taratibu bila onyo, maumivu, wala kujijua. Utadhani unapata usingizi na kujilaza, kumbe ndio mauti yanakukuta. Uthithubutu kupika kwa kutumia mkaa ndani ya nyumba bila kufungua madirisha, au kuwasha jenereta ndani ya nyumba, au kuwasha gari katika “garage” wakati madilisha na milango imefungwa; maana hiyo ni sawa na kucheza na kifo. Gesi ya carbon monoxide ni tofauti na carbon dioxide (CO2) inayopumuliwa na wanyama, ambayo si sumu na inatumiwa na mimea katika photosynthesis.
Miili ya watoto watatu wa familia hiyo
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, June 27, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA RAIS MPYA WA MISRI MHE. ABDEL FATTAH AL-SISI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014
PICHA NA IKULU
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, June 26, 2014

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA HUKO NCHINI EQUATORIAL GUINEA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na ujumbe wa Tanzania kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Mjini Malabo, Equatorial Guinea. Miongoni mwa masuala muhimu yanayotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huu ni bajeti ya umoja huo na mkakati wa kukusanya maoni kutoka nchi wanachama kuhusu Afrika ifikapo mwaka 2063, ambapo umajo huu utafikisha miaka mia moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wajumbe wenzake wa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika unaofanyika Mjini Malabo, Equatorial Guinea.
Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wakiwa kwenye picha ya Pamoja.
Picha na IKULU.
SOMA ZAIDI >>> »

RAIS UHURU KENYATTA NI KINARA KWENYE MTANDAO WA TWITTER BARANI AFRIKA

Rais Kenyatta amempiku Paul Kagame wa Rwanda kwa idadi ya wafuasi kwenye Twitter.
Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika.
Kenyatta amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Kenyatta ambaye amekuwa mamlakani tu kwa mwaka mmoja, amejipatia wafuasi 456,209, yuko mbele ya mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mwenye wafuasi 408,353 ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2000, miaka sita kabla hata ya Twitter kuanzishwa.
Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali mbali, Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia nafasi ya tatu.
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, June 2, 2014

RAIS MPYA WA MALAWI HATIMAYE ATOA HOTUBA YAKE YA KWANZA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa ni miongoni mwa Viongozi wa Kitaifa waliohudhuria na kusikiliza hotuba ya kwanza ya Rais mteule wa Malawi, Prof. Mutharika zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Kamuzu, jijini humo.

Miongoni mwa marais waliohudhuria ni pamoja na Rais Wa Botswana Ian Kama na Waziri wa nje Wa Msumbiji.

Prof. Mutharika aliapishwa rasmi siku ya jumamosi baada ya Tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza rasmi baada ya matokeo ambapo leo rais Mutharika amelihutubia rasmi Taifa hilo kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa jumamosi.

Baada ya Sherehe hizo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Bilal, amekuwa na mazungumzo ya tetea tete na Rais Prof.  Mutharika katika hoteli ya Sunbird. 
 Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal (nyuma) akiwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
 Rais Prof. Mutharika, akiwasili uwanjani hapo akiwa katika gari la wazi.
 Wanahabari wakichacharika kunasa picha na matukio wakati Mutharika akiwasili kwenye uwanja wa Kamuzu Banda.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria.

SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, May 29, 2014

TUME YA UCHAGUZI NCHINI MALAWI KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI KESHO

Taarifa fupi iliyotolewa na tume ya uchaguzi jana usiku mjini Blantyre, imesema wameamua kutangaza matokeo hayo kwa kuzingatia sheria inayoibana kufanya hivyo ndani ya siku zisizozidi nane na ikiwa ni baada ya saa 48 tangu kumaliza hesabu ya kura.Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ameeleza kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe kuwa sasa wananchi wa Malawi wameondolewa hofu ya kusubiri kwa muda mrefu matokeo ya kura za uchaguzi walioufanya juma lililopita.
Kwa siku mbili sasa kumekuwa na tuhuma za kuokotwa kwa baadhi ya masanduku ya kura, huku baadhi ya magari ya yakipatikana na masanduku ya kura na hata katika baadhi ya maeneo ambako ilielezwa kuwa kura zimehifadhiwa, usalama wake umesemwa kuwa mdogo.



Tume ya uchaguzi ya Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi ijumaa.
Tangu jumatatu tume hiyo imekuwa ikisubiri uamuzi wa mahakama kuu mjini Blantyre wa kuiongeza muda wa angalau siku 30 kukamilisha jukumu ililopewa, hata hivyo mahakama yenyewe bado ina mashauri mengine iliyopokea kuhusu uchaguzi huu
Mmoja kati ya wananchi wa nchi hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Malani Nyirenda, alielezea hisia zake alipozungumza na BBC mjini Lilongwe kutokana na suala la kuchelewa kutolewa matokeo na mpango wa kuhesabu upya kura za baadhi ya maeneo.

Tume hiyo imesema hadi kufikia sasa imepokea malalamiko 275 na imekwisha yafanyia kazi malalamiko 170 tu.
Chanzo: BBC Swahili.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, May 24, 2014

RAIS BANDA ASITISHA NA KUYAFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI NCHINI MALAWI


Rais wa malawi Joyce Banda, ametangaza rasmi kusitisha na kuyafuta matokeo ya Uchaguzi uliofanyika nchini kwake kuanzia jumanne ya wiki iliyopita, baada ya Tume ya uchaguzi kuanza kutoa matokeo ya uchaguzi huo ambayo hadi sasa asilimia 30 ya kura hizo inaonyesha Mgombea wa Chama cha upinzani cha Democratic Progressive Party-DP Prof. Peter Mutharika, anaongoza akiwa na jumla ya kura 683, 621.
Anayefuatia kwa kura ni Rais Joyce Banda, wa Peoples Part akiwa na kura 372, 101.
Anayeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo ni Mchungaji Dkt. Lazarus Chakwera, wa Chama cha DPP, akiwa na kura 289, 145, na nayefuatia ni Atupele Muluzi wa Chama cha United Democratic Front-UDF akiwa na kura 269,250.
SOMA ZAIDI >>> »

RAIS JACOB ZUMA AMEAPISHWA KUWA RAIS WA AFRIKA KUSINI MJINI PRETORIA LEO




Rais Jacob Zuma akila kiapo katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria wakati wa sherehe za kuapishwa kwake  leo Mei 24, 2014.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kushuhudia shughuli za kumuapisha Rais Jacob Zuma kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika Jengo la Union Buldings mjini Pretoria leo tarehe 24 May 2014.
 
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiondoka baada ya kumalizika kwa shughuli za kumuapisha Rais Jacob Zuma kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika Jengo la Union Buldings mjini Pretoria leo tarehe 24 May 2014. 

Marais na viongozi toka nchi mbalimbali wakiondoka Union Buildings baada ya kushuhudia Rais Jacob Zuma akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini, leo Mei 24, 2014
 
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, May 22, 2014

WAZIRI AJIPIGA RISASI NA KUJIUA NI BAADA YA KUSHINDWA UCHAGUZI WA BUNGE

 
Naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi amejipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
Godfrey Kamanya alikuwa anayegombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini amejiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.

Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.

Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.

Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe. 
Chanzo : BBC
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, May 12, 2014

BOKO HARAM WAONYESHA WASICHANA WALIOWATEKA

Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara.

Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.

Chanzo: BBC Swahili
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, May 10, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEA KIWANDA KIKUBWA CHA SARUJI KINACHOMILIKIWA NA ALHAJ ALIKO DANGOTE NCHINI NIGERIA

d10
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akipokelewa na mfanyabiashara na muwekezaji mkubwa na maarufu nchini Nigeria Alhaji Aliko Dangote katika kiwanja cha ndege cha kiwanda chake cha cement cha Dangote Cement Obajan Plant kilichopo kilomita 400 kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembelea mnamo tarehe 9 May 2014 na kushoto ni balozi wa Nigeria nchini Tanzania mh. Dkt Ishaya Samalia Majanbu.

d12Rais Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mfanyabiashara na mwekezaji Maarufu nchini Nigeria Alhaji Aliko Dangote,wakati alipokuwa akizungushwa katika kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kinachomilikiwa na mwekezaji huyo tarehe 9 May 2014

d31 (1)Rais Kikwete akitembezwa katika kiwanda cha saruji huku akipata maelezo kutoka kwa wataalamu kutoka katika kiwanda hicho cha Dangote Cement Obajan Plant kinachomilikiwa na mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote wa Nigeria.

d38 (1)Rais Kikwete akitembezwa na Alhaji Aliko Dangote katika sehemu mbalimbali za kiwanda cha saruji kujionea shughuli zinavyofanyika katika kiwanda hicho jana tarehe 9 May 2014. 

 d44 (1)Rais Kikwete akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam wa kiwanda cha Saruji cha Dangote Cement Obajan Plant alipotembelea jana kilomita 400 kaskazini mashariki mwa Lagos.

d48Rais Kikwete akionyeshwa Malighafi zinazotumika kenye kiwanda cha Saruji cha Dangote Cement Obajan Plant alichokitembelea jana.

d49Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitia saini mfuko wa Saruji alipotembelea kiwanda cha Saruji cha Dangote Cement Obajan Plant jana.
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, May 5, 2014

WANAJESHI WAWILI WA DRC KWENDA JERA KWA KOSA LA UBAKAJI


Wanajeshi wa DRC

Wanajeshi wawili wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepatikana na hatia ya ubakaji kati wanajeshi 39 walioshitakiwa kwa makosa ya kivita mashariki mwa nchi hiyo.
Wengine waliobaki wamepunguziwa makosa kutoka makosa ya uhalifu wa kivita lakini wamehukumiwa kwa makosa mengine kama vile uporaji lakini wengi waliachiwa.

 Wanajeshi wa DRC pichani.

Wanajeshi hao wanatuhumiwa kusababisha machafuko yanayoendelea kwenye mji mdogo wa Minova ulio mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2012.
Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23 .
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu wanawake na wasichana 135.
Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la mashariki mwa Congo na yanaidiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili waasi na wale wa serikali.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, May 3, 2014

SHULE NA OFISI KUFUNGWA JUMATANO MJINI ABUJA NCHINI NIGERIA


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathana ameagiza shule zote na ofisi za serikali katika mji mkuu wa Abuja nchini humo zifungwe wakati wa siku tatu za Mkutano wa Uchumi wa Dunia World Economic Forum utakaanza nchini humo jumatano ijayo.
Serikali imesema hatua hiyo ni kuarahisisha misafara ya magari. Lakini suala la kuimarisha ulinzi huenda ni mambo yaliyosababisha hatua hiyo Mwandishi wa BBC Will Ross anasema akiwa Abuja.
Ulinzi mkali umehaidiwa kwa wageni wapatao 1000 wakati wa mkutano huo.
    Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo.
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Marais wa Rwanda, Senegal na Kenya ni miongoni mwa viongozi wa juu wa nchi watakaohudhuria.
Mji wa Abuja katika siku arobaini zilizopita ulishambuliwa kwa matukio mawili ya mabomu yaliyoua watu wapatao tisini na Boko Haram wanahusishwa na mashambulizi hayo.


Baadhi ya wanawake wakiandama kutaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwaokoa wasichana waliotekwa na kundi la Boko Haram

Kundi hilo hilo pia linatuhumiwa kuwateka nyara wasichana zaidi ya 200 katika shule moja kwenye mji wa Borno uliopo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria siku arobaini zilizopita.
Jina la kundi hilo lenye tafsiri ya "Kupiga marufuku elimu ya nchi za Maghiribi" kwa lugha ya Kihausa kimekuwa kikiendesha mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Nigeria katika siku za hivi karibuni.


Wanawake walivaa nguo nyekundu kuonyesha kuguswa na wasichana waliotekwa

Inakadiriwa watu wapatao 1500 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo pamoja na operesheni ya majeshi ya serikali wakati wa kulisaka kundi hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ambaye anafanya ziara barani Afrika amesema Marekani itafanya kila liwezekanalo kuisaidia serikali ya Nigeria kuwaokoa na kurudisha nyumbani wasichana mia mbili waliotekwa na kundi la waislamu linalosadikiwa kuwa la Boko Haram siku kumi tisa zilizopita.
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, April 30, 2014

MORGAN TSVANGIRAI AMTIMUA HASIMU WAKE



Morgan Tsvangirai

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai aliyetimuliwa kutoka katika uongozi wa chama chake cha MDC amesema kuwa hasimu wake katika chama hicho Tendai Biti, naye ametimuliwa pamoja na wanachama wengine 8.
'Bwana Biti ni mtegemea tu cha wengine ambaye anatumiwa na rais Robert Mugabe,'' alisema Tsvangirai.
Mnamo siku ya Jumamosi, mrengo mmoja wa chama hicho unaoongozwa na Biti ulisema kuwaTsvangirai, alisimamishwa uongozi wa chama kwa muda, kwa sababu ya kukosa uwezo wa kuongoza chama hicho.
Mgawanyiko katika chama cha MDC, unakuja baada ya chama hicho kushindwa vibaya katika uchaguzi uliofanyika 2013.
Uchaguzi huo ndio ulikuwa mwisho wa muungnao uliokuwepo kati ya chama tawala Zanu-PF na MDC ulioundwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2008 uliokumbwa na utata.
Tsvangirai na Bwana Biti, ambaye ni katibu mkuu wa chama cha MDC walikuwa washirika kwa muda mrefu katika kampeini yao dhidi ya Mugabe, ingawa walitofautiana Julai mwaka jana.
Tsvangirai alisema Biti na wanachama wenzake aliowaita waasi, wameondolewa katika vyeo vyao kama wabunge.
"alituhadaa, Mwanamume huyu hata haamini chochote isipokuwa mamlaka,'' alisema Tsvangirai kuhumusu Biti.
Mnamo siku ya Jumamosi mrengo wa bwana Biti ulisema kuwa baraza la chama cha MDC lilipiga kura kumondoa Tsvangirai kutoka katika uongozi wa chama hicho, wakisema kuwa chama hicho kimeguzwa na kuwa kama himaya ya mtu mmoja.
Kwa upande wake Tsvangirai alipuuza mkutano huo kama usio halali na ulio kinyume na katiba
Wafausi wengi wa MDC, wana wasiwasi kuwa malumbano hayo yanaweza kuimarisha utawala wa Mugabe na chama chake na wanatumai kuwa wataweza kusuluhisha tofauti zao.
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, April 25, 2014

WATU KADHAA WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUTOKEA MKANYAGANO NCHINI DRC



 
  Marehemu Emeneya anasifika kwa kuanzisha utumizi wa zana za elektroni katika muziki nchini DRC

Watu kadhaa wameripotiwa kufariki baada ya kutokea mkanyagano katika tamasha la kumkumbuka mwanamuziki maarufu wa Congo King Kester Emeneya.
Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki ingawa maafisa wakuu bado hawajatoa takwimu rasmi za watu.
Maafisa wanasema kuwa mwanamuziki huyo alifariki mjini Paris mapema mwaka huu akiwa na umri wa miaka 57.
Idadi kubwa ya watu ilikusanyika nyumbani kwake mjini Kikwit katika Jamhuri ya kidemokrasia kwa tamasha hilo la kumkumbuka.
Maelfu walihudhuria mazishi ya marehemu nyumbani kwake karibu na mji wa Kinshasa mwezi Machi baada ya kifo chake mwezi Februari kutokana na maradhi ya Moyo.
Shirika la habari la AFP limesema kuwa Emeneya alikuwa mwanamziki mbunifu aliyeanzisha utumizi wa zana za kielektroniki katika muziki nchini Congo.
Tamasha hilo lililotarajiwa kuendelea hadi Jumapili limefutiliwa mbali
SOMA ZAIDI >>> »