Pages

Showing posts with label Yanga. Show all posts
Showing posts with label Yanga. Show all posts

Friday, March 13, 2015

VIINGILIO MECHI YA YANGA SC DHIDI YA FC PLATNUM VYATAJWA

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ametoa taarifa ya viingilio kwa mchezo wa keshokutwa dhidi ya FC PLATNUM ambapo katika jukwaa la viti vya Rangi Chungwa itakuwa Sh, 7,000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh. 20,000, na VIP A Sh 30,000.
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi Saa 2:00 asubuhi katika vituo vya Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).Aidha, amesema magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya Uwanja siku ya Jumapili.
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, November 26, 2014

MBRAZILI MPYA WA YANGA EMERSON DE OLIVERIA NEVES ROUQE ATUA DAR LEO KWA MAJARIBIO

Nyota mpya wa Klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam, anayekuja kufanya majaribio ya kuziba nafasi ya Mbrazili mwenzake Genlson Santos 'Jaja', Emerson De Oliveria Neves Rouqe akitoa ishara ya dole mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa Yanga. Rouque aliwasili na Kocha mkuu wa Yanga, Marcio Maximo pamoja na Nyota mwingine kutoka Brazili  Andrew Coutinho.
SOMA ZAIDI >>> »

Saturday, November 8, 2014

LIGI KUU TANZANIA BARA: YANGA YAICHAPA MGAMBO MABAO 2-0

Mshambuliaji Saimon Msuva akishangilia moja ya mabao aliyofunga leo dhidi ya Mgambo JKT, kushoto ni Ngasa na kulia Dilunga
Pamoja na kuonyesha soka safi, Mgambo Shooting ya Tanga imeshindwa kuhimili mikiki ya Yanga na kukubali kipigo cha mabao 2-0.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga walipata mabao yao yote kupitia kwa Simon Msuva katika dakika ya 73 na 90.
Kabla ya mechi hiyo, Yanga ilikuwa imepoteza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Licha ya kumkosa nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro', Yanga ilionyesha soka safi huku soka lake likiwa ni la kuvutia.
Mgambo nao walikuwa wakipeleka mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga lakini hawakuwa makini kwenye umaliziaji.
SOMA ZAIDI >>> »