Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu,
Mama wa Mtoto akiwa hospital baada ya kuzimia.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo
ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha
Chanzo:local media
Chanzo:local media
No comments:
Post a Comment