Pages

Showing posts with label Elimu. Show all posts
Showing posts with label Elimu. Show all posts

Saturday, November 1, 2014

FAHAMU KUHUSU HOMA YA MANJANO

Homa ya manjano ni tatizo linaosababisha ngozi yako, midomo na sehemu nyeupe ya jicho kuwa ya njano kutokana na kuongezeka kwa rangi ya bilirubini katika damu inayotengenezwa kwenye ini baada ya kuvunjwa kwa seli nyekundu za damu.

 Hali hii inaweza kuambatana na kinyesi cheye rangi ya udongo mfinyanzi au kutoa mkojo mweusi, mwili kuwasha, kutapika kukosa hamu ya kula na uchovu. 

NINI INASABABISHA
Tatizo ili sio ugonjwa bali ni ishara kuonyesha kuna kasoro inayo sababishwa na mojawapo kati ya yafuatayo:-
Ugonjwa sugu wa ini (Liver Cirrhosis)
Magonjwa ya damu na upungufu wa damu.
Homa ya ini
Kuziba kwa mirija ya nyongo
Kuwepo kwa mawe kwenye nyongo 
Maambukizi na matumizi ya dawa za kutibu magonjwa mbalimbali kwa muda mrefu.
Kuvimba kwa ini kutokana na matumizi ya pombe na sigara kwa muda mrefu.
MATIBABU
Baada ya kufanyiwa uchunguzi na vipimo vya mkojo, ini, ultrasound, MRI tiba hufanyika kutokana na nini kinasababisha ambapo inaweza kuwa ni dawa, upasuaji au kuongezewa damu ili kuzuia tatizo la ini kushindwa kufanya kazi na kifo.
Tatizo ili pia linaweza kuzuiwa kwa kupata chanjo ya homa ya ini, kuepuka uvutaji wa sigara, pombe kupita kiasi na kupunguza uzito.
Kunywa juisi ya papai, nyanya au majani ya mpapai glasi moja kila siku asubuhi yana Lycopene ambayo huzuia kuharibika kwa ini.
Kausha na changanya majani ya matango kwenye chai mara 3 kwa siku au unaweza kula matango mara kwa mara.
Kunywa juisi ya majani ya kunde au mbaazi kila siku au unaweza kutafuna mbegu zake.
Pia juice ya miwa, limao na tangawizi ambazo zimetengenezwa nyumbani zitasaidia ini kufanya kazi vizuri
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, October 27, 2014

JE! UNA UFAHAMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA?


Ugonjwa wa Ebola unasababishwa na Virusi na ni ugonjwa hatari unaoambukiza haraka binadamu na wanyama mwitu (hayawani) kama kima, sokwe, popo, ndege, mijusi, amfibia, na kadhalika. Ugonjwa huu unaosababishwa na virusi aina ya Ebola Virus ni wa mlipuko.
Japokuwa hakuna mazingira maalum ambamo virusi vya Ebola vinapatikana, lakini wataalamu wanasema virusi hivyo vinapatikana kwa mnyama ambaye anapatikana zaidi barani Afrika.
Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi nyingi na bado unaendelea kupukutisha maisha ya watu wengi hasa barani Afrika. Matukio ambayo yamethibitishwa kuwepo kwa ugonjwa huo ni katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea, Ghana, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Sudan, Ivory Coast, Uganda na kadhalika.

 
Ugonjwa wa Ebola daima unasambaa ndani ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya.Hata hivyo, matukio mengine yamekuwa yakitokea nje ya maeneo hayo na hayafahamiki.
Jinsi ugonjwa huo unavyosambaa:
Namna ugonjwa huo ulivyojulikana kwa mara ya kwanza hakuna anayefahamu kwa hakika. Hata hivyo, ugonjwa wa Ebola unaweza kusambazwa kwa njia zifuatazo:
1. Kugusana moja kwa moja na mtu ama mnyama mwenye ugonjwa huo;

2. Kugusana moja kwa moja na damu ama majimaji (mate au mafua) ya mtu mwenye ugonjwa huo katika familia;

3. Kugusa vifaa vya tiba vilivyo na virusi vya ugonjwa huo kama sindano;

4. Kutumia vifaa visivyochemshwa katika hospitali kama sinano;

5. Kula ama kushika vinyesi vya wanyama wenye ugonjwa huo;

6. Kuvuta hewa yenye virusi vya ugonjwa huo katika mazingira ya hospitali;

7. Kutumia nyama ya wanyama walioathirika kama kitoweo;
8. Kutozingatia tahadhari za kitaalam.

Dalili za Ebola:
Mtu au mnyama mpaka aonyeshe dalili za ugonjwa wa Ebola huchukua kati ya siku 2 hadi 21. Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na:
1. Homa kali
2. Kuumwa kichwa

3. Kuharisha

4. Kutapika

5. Maumivu ya kifua

6. Maumivu ya tumbo

7. Mafua

8. Kikohozi
9. Maumivu ya misuli na viungo, hasa kwenye viungio
10. Kuvimba koo
11. Mwili kuwa dhaifu
12. Mfadhaiko
13. Kuchanganyikiwa
14. Macho kuwa mekundu
15. Kuvuja damu kwa ndani na nje

Nani aliye katika hatari?
1. Watu wanaofuga wanyama mwitu ama wanaoishi katika maeneo yenye wanyama mwitu;

2. Watu wanaotegemea wanyama mwitu kama popo kama chakula chao;

3. Watumishi wa vyumba ya kuhifadhia maiti;

4. Watumishi wa afya wanaowahudumia wagonjwa wa Ebola;

5. Watumishi wa afya katika hospitali ambazo hazina mazingira bora na safi;

6. Wanafamilia wa wagonjwa wa Ebola;

7. Watu wanaohudhuria hospitali ambazo hazina mazingira safi na salama;

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola:
1. Epuka kugusa damu/majimaji ya wanyama ama binadamu walio na ugonjwa wa Ebola au hata maiti za watu waliokufa kwa ugonjwa huo kwa kuzingatia haya:
a) Tunza mazingira safi na salama ya hospitali;

b) Watelekeze wagonjwa wa Ebola;

c) Fukia miili ya waliokufa kwa Ebola kwa usalama;

d) Epuka mazishi ya kienyeji kama kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola;

2. Watumishi wa afya na wanaowatazama wagonjwa wa Ebola wanatakiwa:
a) Kuvaa kwa usahihi vifaa vya kujikinga na nyuso, mikono na macho,

b) Na majoho maalum daima;

c) Kutumia sindano mara moja na kuziteketeza ama kuzifukia;

d) Epuka kutumia zaidi ya mara moja sindano au kutotumia sindano ambazo hazijachemshwa vyema;

e) Epuka kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola;
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, September 18, 2014

VYAKULA VINAVYOSABABISHA SARATANI

UTAFITI mbalimbali uliokwishafanywa unaonyesha kuwa magonjwa mengi ya saratani (cancer) yanatokana na vyakula tunavyokula kila siku katika maisha yetu. Katika siku za hivi karibuni, ongezeko la magonjwa haya limekuwa kubwa kwa sababau vyakula vinavyosababisha magonjwa hayo, ndivyo vinavyoliwa sana kuliko vile vinavyozuia.
 Wiki iliyopita tuliwaorodheshea baadhi ya vyakula vinavyoaminika kusaidia kuzuia magonjwa ya kansa ambapo wiki hii tunawaletea orodha ya vyakula vinavyoaminika kuongoza kwa kuwa chanzo cha magonjwa hayo hatari:
VYAKULA VYA KUKAANGA
 Vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya na miongoni ma madhara hayo ni pamoja na kusababisha kansa ya kwenye mfuko wa uzazi. Vyakula hivyo ni pamoja na chips na vyakula vingine vinavyopikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.
VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI
 Vyakula vyenye chumvi nyingi vimebainika navyo kusababisha kansa. Vile vile inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa kansa tumboni. Kansa ya tumbo inadaiwa kuua watu wengi nchini Japan kutokana na jamii hiyo kupenda sana vyakula vyenye chumvi nyingi. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni vile vya kusindika, kama vile nyama za makopo, maharage, n.k
SUKARI
 Matumizi mabaya ya sukari yanaelezwa kusababisha kansa. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa kwenye vinywaji mbalimbali, zikiwemo soda, juisi za ladha ya matunda ambazo huwa na kiwango kingi cha ‘fructose’ ambayo inaelezwa kusababisha saratani ya kongosho.
 Vile vile sukari kwa ujumla wake hairuhusiwi kutumiwa na mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na kansa kwa sababu chakula cha chembechembe za saratani mara nyingi huwa ni sukari. Kwa matumizi mengine ya kawaida, sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula tunavyotumia, tofauti na baadhai ya watu wanavyoweka sukari nyingi ili kupata utamu zaidi.
NYAMA ILIYOIVA SANA
 Upikaji wa nyama kwa muda mrefu na kwenye moto mkali (high temperatures) husababisha aina fulani ya kemikali inayojulikana kitaalamu kama ‘heterocyclic aromatic amines’. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah (University of Utah), umeonesha kwamba watu wanaopenda kula nyama zilizoiva sana, wako hatarini zaidi kupatwa na saratani ya njia ya haja kubwa (Rectal Cancer). Hivyo inashauriwa unapopika nyama, usipike kwenye moto mkali na kuiva kupita kiasi.
POMBE
 Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake kwa waume. Aina ya saratani zinazodaiwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya mdomo, ini, utumbo na koromeo, ambazo ndizo zinazoua watu wengi hivi sasa nchini Marekani.
NYAMA NA MAFUTA
 Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja. Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.
 Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu husababisha saratani pia. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa ya saratani.
VYAKULA VYA UNGA MWEUPE
Vyakula vyote vinavyopikwa kutokana na unga uliokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake vyote na kuwa mweupe, vinaelezwa kuchangia magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘donati’ (doughnuts), maandazi, mkate mweupe, n.k
 Mwisho, licha ya kuepuka ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu, unatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. Utaona kwamba adui mkubwa wa afya zetu ni vyakula vyote vya kusindika na vile vya kutengenezwa viwandani au vile ambavyo wakati wa utayarisjaji wake huondolewa virutubisho vyake vya asili.
SOMA ZAIDI >>> »