Pages

Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

Friday, October 31, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEWA NA VIONGOZI WA BENDI YA MSONDO NGOMA IKULU LEO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja  na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu leo na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro).
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, October 30, 2014

MWANA FA AMKUBALI SANA ALI KIBA

Staa wa muziki wa Bongo fleva tangu kitambo Hamisi Mwinjuma aka Mwana FA  amefunguka kuwa kati ya wasanii anaowakubali hapa Bongo ni pamoja na Alikiba akipiga story na chanzo makini cha habari mwana FA anaye bamba na ngoma ya ‘Kiboko yangu’ aliyo mshirikisha Ali Kiba aliseama kuwa

Ujue Ali Kiba ana sauti ile ambayo huwa naitaka ndio maana ngoma yangu hii mpya ‘Kiboko yangu’ kaitendea haki siku zote katika nyimbo zangu huwa sijali msanii anajina kiasi gani bali huwa naangalia uwezo alionao na mfano mkubwa nimeuonesha kwenye wimbo wa Mfalme nilio mshirikisha G Nako.
SOMA ZAIDI >>> »

KESI DHIDI YA LUNDENGA KUMEKUCHA TENA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemruhusu Prashant Patel kubadilisha hati ya madai katika kesi aliyoifungua dhidi ya mshirika wake, Hashim Lundenga.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Frank Moshi, amemruhusu Patel kupitia wakili wake Benjamin Mwakagamba wa kampuni ya Uwakili ya BM, baada ya kuiomba mahakama hiyo kufanya hivyo ili aweze kuingiza gharama ambazo zilijitokeza baada ya kufanyika kwa shindano la Miss Tanzania, Oktoba 11, 2014.

Hata hivyo Hakimu Moshi alimtaka Patel kufanya mabadiliko ya hati hiyo ya madai dhidi ya Lundenga na kuiwasilisha mahakamani hapo kabla ya jana Jumatano.

Baada ya kuruhusu Patel kubadilisha hati hiyo ya madai, Hakimu huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 3 kwa ajili ya kutajwa.

Patel amechukua hatua hiyo baada ya maombi yake ya kutaka kuzuia shindano hilo la Miss Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Jumamosi ya Oktoba 11, 2014 kushindikana.

Mshiriki huyo mwenza wa Lundenga kupitia wakili Mwakagamba, waliyafungua maombi hayo ya kuomba zuio hilo la shindano la Miss Tanzania chini ya hati ya dharura.

Katika maombi yake, Patel anadai Lundenga alikuwa na mpango wa kuendesha shindano hilo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, kinyume cha sheria na bila hata ya kumwarifu.

Hivyo aliiomba mahakama itoe zuio la kufanyika kwa shindano hilo hadi shauri la msingi alilofungua litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Katika kesi yake ya msingi, Patel anadai pamoja na mambo mengine, utekelezaji wa makubaliano ya Februari 20, 2012 na malipo ya Sh19 milioni ambayo hayajalipwa kwa mujibu wa mkataba wao na faida nyinginezo ambazo zimejitokeza hadi Septemba 23, mwaka huu.

Kupitia hati yake ya kiapo inayounga mkono maombi yake, Patel anadai kuwa yeye na Lundenga ndio waanzilishi, waongozaji na waendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania na wamekuwa katika hali hiyo kwa miaka 20 sasa, tangu yaliporuhusiwa tena 1994.
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, October 29, 2014

ALICHOANDIKA DIAMOND PLATNUMZ INSTAGRAM KUHUSU KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU(PHD) NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM(UDSM)

Photo: => Uamuzi wako ndio Mafanikio yako ama kufeli kwako...Zingatia!

=> Your decision is your success or your failure ... Note!

TANGAZO NDUGU ZANGU:
Ifikapo Tarehe 8 Novemba Saa 10 jioni,Kijana mwenzetu ambaye sisi tunamdharau na wengine wapuuzi kabisa kwa kufeli kwao maisha wana wivu na wanathubutu kumzomea atakuwa anatunukiwa Shahada ya Uzamivu(Phd) na Chuo Kikuu Cha Dar es S
alaam(UDSM) kwa kuthamini mchango wake kwenye jamii...Honorary Phd hata Raisi wetu anayo...Alongside DIAMOND mwingine atakayepewa Shahada hii ya Heshima kwenye Mahafali haya ni Balozi Fulgence Kazaura ambaye amewahi kuwa VC wa UDSM miaka ya nyuma!!
Ningependa kuwakaribisha wale Wazomeaji woooteee wenye sauti mbaha kabisa waweze kufika kwenye Viwanja vya UDSM kushuhudia Tukio la Kihistoria kwa Mtoto huyu wa Tandale ambaye ni BIDII NA HESHIMA Vimemfikisha hapa..
SHKAMOO DR.NASIBU ABDUL au Pengine DR.DIAMOND PLATNUMZ au ukitaka swaga DR.PLATNUMZ BABY!
Sky is never the limit!Hongera kwa Mameneja waliomfikisha DIAMOND hapo alipo @babutale @mkubwafella na @sk_ent
Kudos bro @diamondplatnumz
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, October 27, 2014

LULU AITAMBULISHA RASMI FILAMU YAKE MPYA 'MAPENZI YA MUNGU'

 Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.
 Msanii Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA MUNGU.
Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.

Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. 


Akiongezea kuwa..."Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo"
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana  katika Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni Leo.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.

Chanzo: Jiachie blog
SOMA ZAIDI >>> »

Sunday, October 26, 2014

LUNDENGA AKANUSHA KUJIVUA TAJI LA MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU

MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014).Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru.

“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.

Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.
“Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo nab ado tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.
SOMA ZAIDI >>> »

ALI KIBA AKANUSHA KUANDAA WATU KUMZOMEA DIAMOND PLATNUMZ

Alikiba amekanusha uvumi unaodai kuwa huenda aliaandaa watu maalum wa kumzomea Diamond Platnumz kwenye show ya Fiesta iliyofanyika October 18 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Alikiba amesema kuwa hajui uvumi huo umeanza vipi.
“Hamna ukweli wowote, naanzaje?,” amehoji. “Siwezi kufanya kitu kama hicho. Kikubwa ni kuwashukuru wana Dar es Salaam walivyonipokea, nimefurahi sana. Hii imenitia moyo na kunifanya niongeze bidii kuwaandalia vitu vizuri zaidi.”
Katika hatua nyingine, msanii huyo amesema mashabiki wa muziki wake wasishangae kuona video ya wimbo wa ‘Mwana’ wiki hii ama wiki ijayo. “Video ni muda wowote yaani, usishangae ukasikia video imetoka. Muda wowote video inatoka surprise, kwahiyo waendelee kusubiri muda wowote.”
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, October 24, 2014

KAULI YA MISS TANZANIA No. 3 KUHUSU YANAYOENDELEA KWA MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU

Miss Tanzania namba tatu, Jihan Dimachk. 
Yameongelewa mengi na kimsingi mpaka sasa bado ushindi wake unaonekana kuwa na makengeza. Kutokana na hali hiyo, waandishi wetu walifanya mazungumzo na baadhi ya wadau lakini kati yao alikuwa mmoja wa washiriki ambaye alichukua nafasi ya tatu, huyu ni Jihan Dimachk. 
Gumzo mtaani kwa sasa kwenye ulimwengu wa urembo ni ushindi wa mwanadada Sitti Abbas Mtevu ambaye hivi karibuni aliibuka mshindi katika Shindano la Miss Tanzania 2014. Tutakumbuka baada ya Sitti kutangazwa mshindi, maneno yalikuwa mengi, mara alipendelewa, mara alidanganya umri, wengine wakasema eti ana mtoto. 
Kwenye fainali za mashindano hayo mrembo huyu alichukua Taji la Miss Tanzania Top Model 2014 na sasa fuatilia exclusive enterview hii iliyofanyika kati yake na Ijumaa ndani ya Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni, Dar. 
Ijumaa: Habari yako Jihan, sisi ni waandishi kutoka Gazeti la Ijumaa.
Jihan: Okey, nashukuru kuwafahamu, karibuni. Ijumaa: Tuanze na matokeo ya kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huu, unadhani wewe ulistahili kuchukua nafasi ya tatu na Sitti Mtemvu kuibuka kidedea?
Jihan: Siwezi kuongea sana jamani lakini kwa kifupi nilikuwa nikiamini nitashinda, niseme tu kwamba it was unfair but I can’t explain (haikuwa sawa ila siwezi kuelezea).
Ijumaa: Kwa nini unasema hivyo? hebu fafanua kauli yako.
Jihan: Sipendi kuwa muongeaji sana, naheshimu maamuzi ya majaji na Kamati ya Miss Tanzania lakini ukweli uliopo moyoni mwangu ni kwamba nilijiamini na ndiyo maana niliingia kwenye kinyang’anyiro nikijua ushindi ni haki yangu.
Ijumaa: Wapo wanaosema ulikuwa na kila kigezo cha kuwa Miss Tanzania 2014 lakini umetoswa kutokana na rangi yako ukihisiwa wewe si Mtanzania, unaliongeleaje hili? Jihan: Sipendi kabisa kusikia maneno hayo, mimi ni Mtanzania, nimezaliwa Mwanza, mama yangu ni Msukuma na baba yangu Mlebanon. Tangu naingia kwenye shindano hili waandaaji walinihoji, wakafuatilia hilo na kutambua ni Mtanzania, ingekuwa tofauti sidhani kama ningeruhusiwa kushiriki.

Ijumaa: Kwa mfano ikitokea Sitti akavuliwa taji kutokana na haya yanayozungumzwa, uko tayari uvishwe wewe?
Jihan: Siwezi kulijibu swali hilo kwani haijatokea. Endapo itatokea na waandaaji wakanifuata kuniambia hivyo, hapo ndiyo nitakuwa na la kuzungumza. Ijumaa:Unamuongeleaje Sitti Mtemvu? Jihan: Kwa sababu ndiye aliyevishwa taji, naheshimu ushindi wake, namkubali kuwa ni mrembo na siwezi kupingana na maamuzi yaliyotolewa.
Ijumaa: Umechukua nafasi ya tatu ambayo nayo si haba, una mipango gani ya baadaye? Jihan: Nina mambo mengi ya kufanya. Nina ndoto za kuwasaidia wanawake na watoto lakini pia nahisi nina jukumu la kusaidia katika suala la elimu nchini, nitajipanga kufanikisha hayo. Ijumaa: Kwa nini elimu?
Jihan: Nimekuwa nikikutana na watu wengi ambao elimu imekuwa kikwazo kwenye maisha yao, nikawa nimejiapiza kuhakikisha nawasaidia kadiri nitakavyoweza. Ijumaa: Asante sana Jihan, tunakutakia mafanikio katika yale unayopanga kuyafanya.
Jihan: Nashukuru sana.

Chanzo:Global publisher
SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, October 23, 2014

NEW AUDIO: Mwana FA (@MwanaFA) ft. Ali Kiba (@OfficialAliKiba) – KIBOKO YANGU

Mwana FA na Alikiba
Sote tumeusubiri kwa hamu na sasa wimbo mpya kabisa wa Mwana FA na Alikiba umewasili rasmi. Baada ya Mwana FA kutoa wimbo wa Mfalme live katika tuzo za KTMA 2014 msanii huyu ameungana na mfalme wa bongo flava yaani Alikiba ili kuwaletea mashabiki wake kazi nyingine kali. Producer wa wimbo huu si mwingine bali ni Marco Chali wa kutoka MJ Records ya jijini Dar Es Salaam. Katika kuurekodi wimbo huu kumekuwa na matoleo manne tofauti ambayo wadau walikuwa wakisindwa kuamua ni upi wa kuachia kwa kuwa zote zimesimamia kucha. Mwana FA na kampuni ya LifeLine ambaye yeye pia ni mkurugenzi wameamua kuuachia wimbo huu moja kwa moja kupitia Mkito.com ili kuhakikisha unawafikia wapenzi wake wengi zaidi na kuhakikisha kuwa kuna maslahi yanapatikana katika kazi hii. Pakua wimbo huu mpya kabisa sasa upate flava kali.

SOMA ZAIDI >>> »

WEMA SEPETU APONDA RAHA NDANI YA CHINA

WAKATI bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya kuzomewa na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Wema Sepetu ‘Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China, Amani lina full data.Bebi wa mbongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ , Wema Sepetu ‘Madam’. Chanzo makini kilicho ‘kloz’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini, kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha la Fiesta, akiwa
ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake, Martin Kadinda na Petit Man, wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo. Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou nchini humo, Wema na wanaume hao wawili walichukua vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn, inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China. 
“Yaani Wema jamani ana mambo, inavyoonekana lile rhumba la wakati ule ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho inauma. Wewe fikiria mtu amekwenda kuchukua vifaa vya biashara, unakwenda na hao wanaume wa kazi gani kama siyo kupoteza fedha tu,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu ‘Madam’ akipozi. Inadaiwa kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi kuliko yoyote duniani, ni ununuzi wa vipodozi, kwani ana mpango wa kufungua duka kubwa katika eneo ambalo halijatajwa jijini Dar es Salaam. 

Baada ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi maisha ya starehe, wakila bata katika klabu mbalimbali za usiku, ambako wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha. 

“Kwa matanuzi anayofanya kule, hata hiyo biashara aliyoifuata haina maana, angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli, angetafuta tu hoteli ya kawaida ili kubana matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa, sasa wewe mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa, tena na wanaume wawili wanakutegemea, hizo pesa si kuzitapanya tu jamani,” kilisema chanzo hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo
SOMA ZAIDI >>> »

Wednesday, October 22, 2014

PICHA ZA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUACHIWA KWA DHAMANA LEO


.
Taarifa zinazomhusu msanii Diamond Platnumz kuhojiwa na jeshi la Polisi hii leo zimeenea sana kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kuanzia jana (tarehe 21 Oktoba) meneja wa msanii huyo Babu Tale amekua akihojiwa na polisi mpaka alipoachiwa kwa dhamana mapema leo saa 5.
.
Vile vile msanii Diamond aliripoti polisi mapema leo kwa ajili ya kuhojiwa, ambapo baada ya kuhojiwa msanii huyo ameachiwa kwa dhamana pia jioni hii. Hizi ni picha zikimuonesha msanii Diamond akitoka kuhojiwa na jeshi la polisi.

.
.

.
.

.
.

. 

                                          Chanzo: Millard Ayo

SOMA ZAIDI >>> »

MADANSA WA DIAMOND WAKAMATWA

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' , akitoa burudani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2014, Leaders Club jijini Dar.
Madansa wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinum wamekamatwa leo wapo kituo cha polisi cha Oyster Bay, Dar kwa kuvaa sare za JWTZ.
Wakati huohuo polisi  wakiendelea kumtafuta bosi wao Nasibu Abudul ' Diamond Platinumz kwa maelezo zaidi kutokana na kuvaa sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ) katika tamasha la Serengeti Fiesta Leaders Club, Dar usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita, hawajampata.
Mwandishi wetu alimtafuta Meneja wa  Diamond aitwaye Babu Tale kwenye simu bila mafanikio.
Chanzo Global publisher
SOMA ZAIDI >>> »

Q-CHILLA AZUNGUMZIA KUHUSU BIFU KATI YA ALI KIBA NA DIAMOND PLATNUMZ

Mapya yanazidi kuibuka kuhusu ushindani wa Diamond na Ali Kiba amba ulianzia katika hitimisho la tamasha la Fiesta lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club Dar. Mashabiki wa wasanii hawa wawili wanavutana huku kila mmoja akisema 

mwenzake ana kipaji na anamfunika mwenzake. Inasemekana kua kuna baadhi ya mashabiki walikodiwa kwa ajili ya kumzomea Diamond wakati akitoa burudani siku ya Fiesta na hilo lilithibitishwa na Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond.

Tumepata bahati ya kufanya mahojiano na Q Chief na haya ndio mahojiano yetu na Q Chief
Mwandishi : kwa sasa katika mziki wa BongoFlava kumekua kuna fitini nyingi wakati mwingine wasanii kwa wasanii wanachonganishwa na mwisho wa siku unakua ugomvi, kwa mfano sasa hivi bifu la Ali Kiba na Diamond. Je Q Chie unalizungumziaje hili

Q Chief : Yote wanayopitia ni changamoto ambazo pengine hawakuwahi kuzania kwamba watapitia. Mi nmepitia situation ambazo zimenijenga kua sugu na Legendary ndio maana ya kua mkongwe unapitia situation ambazo watu wengine wanakufosi ufike huko. Hata kama upo level fulani wanakushusha kwa kufikiria kwamba wanaweza kukushusha. unapandishwa na watu, unapandishwa na mwenyezi Mungu, unashushwa na watu, unashushwa na mwenyezi Mungu. Mfano nimekua nikiangalia Fiesta kwenye TV sikwenda kwa sababu nlikua na mambo yangu Studio, hakuna kitu kigeni nlichokiona, nmeona msanii wa marekani anafunikwa na msanii wa Tanzania ambaye ni Ali Kiba. Nmeona Ali Kiba ambaye amekaa kimya kwa miaka mitatu bila Airtime na watu wamemzungumzia vibaya, vizuri na nini wamemkubali tena. Ikiwa ni mtu yule yule ambaye wamemkataa na wakumuweka mtu mwingine juu. Hakuna kitu kisichowezekana, matokeo uliyoyaona juzi ndio matokeo yanayotokea na yataendelea kutokea. Hakuna Mungu wa hii kazi, hakunaga mfalme wa hii kazi ila kuna masultan wa Hii Kazi.
SOMA ZAIDI >>> »

JOKATE AMPIGIA DEBE DIAMOND PLATNUMZ


Wakati akiandamwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuvaa sare za jeshi hilo bila ruhusa maalumu, msanii wa muziki wa kipya nchini, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond amepigiwa chapuo na mtangazaji wa kituo cha Channel O, Jokate Mwegelo.
Mwegelo amewataka Watanzania kumpigia kura Diamond katika shindano la tuzo ya video bora Afrika inayofanyika nchini Afrika Kusini.


Alisema Watanzania wanatakiwa kuweka uzalendo mbele kwa kumpigia kura msanii huyo kwani ushindi wake utaisaidia Tanzania kuzidi kujulikana kimataifa katika sekta ya muziki na hata katika masuala mengine ya utamaduni.

SOMA ZAIDI >>> »

Tuesday, October 21, 2014

MWAKILISHI WA KENYA ATIMULIWA KUSHIRIKI BIG BROTHER

 
Baada tu ya wiki mbili katika nyumba ya Big Brother Mwakilishi mmoja wa Kenya Sabina ametimuliwa.
Sabina ana mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo.



Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa makala hiyo waliamua kumuondoa Sabina baada ya siku 14 pekee ili aende kumuhudumia mwanawe

Sabina alionekana kumkosa sana mwanawe na wakati mwingi alionekana akifunga vitu kwenye mgongo wake ungedhani anambeba mtoto.
Aliweka pamoja blanketi na nguo na kuvifunga kwenye mgo wake akiwa na kofia ya mwanawe huku akitembea katika nyumba hiyo kabla ya kujiunga na wenzake waliokuwa wakijivinjari nje.

Baadhi wanasema kufunga vitu mgongoni ndio chanzo za mashabiki kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani kwa mwanawe mwenye miezi minane.

Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka katika Big Brother house.
Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lilian kutoka Nigeria na Esther wa Uganda.
Hatua ya kumondoa Sabina katika Big Brother house inamwacha mwakili mmoj tu wa Kenya Melvin Alusa ambaye ni kakake Ben aime Baraza wa kikundi cha wanamuziki cha Sauti Sol.

Credits: Baabkubwa Magazine
SOMA ZAIDI >>> »

MAMA YAKE MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU AONGELEA KUHUSU KASHFA YA UMRI WAKE

 

Kwa kashfa na maneno yote yanayosemwa juu ya binti yake, Sitti Mtemvu, si jambo la kuuliza mara mbili iwapo mama yake anaweza kuwa na urafiki na vyombo vya habari.
Mama mzazi wa Miss Tanzania 2014 alipata fursa ya kuwapa makavu live waandishi wa habari waliotaka kufahamu mtazamo wake kuhusiana na skendo ya kudanganya umri inayomhusu mwanae. jionee hapo chini.


SOMA ZAIDI >>> »

LUNDENGA HATIMAYE AMEHITIMISHA RASMI SUALA LA UTATA WA UMRI WA MISS TANZANIA 2014 SITTI ABBAS MTEMVU

 Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo 


"Katika mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema Lundenga mbele ya wanahabari hao.


Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
 Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala ya cheti cha kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wazazi wake.
 Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991.
Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa habari. 

Chanzo: Jiachie
SOMA ZAIDI >>> »

JE, SITTI MTEMVU KUVULIWA TAJI LA MISS TANZANIA 2014 LEO?


Kamati ya Miss Tanzania leo inatarajiwa kuelezea ukweli juu ya sakata la kudanganya umri la mshindi wa taji hilo mwaka huu, Sitti Mtemvu.

Mratibu wa shindano hilo Hashim Lundenga amesema kamati yake itaelelezea taarifa ambazo walikuwa nazo kuhusiana na mrembo huyo na matokeo ya uchunguzi baada ya taarifa nyingi zilizoibuka.


"Yamesemwa mengi na yameandikwa mengi, hivyo leo itajulikana kama atavuliwa taji ama la" maneno hayo amesema Lundenga
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, October 20, 2014

MANENO YA MSANII DAVIDO KUHUSU FIESTA KUPITIA UKURASA WAKE WA INSTAGRAM

Msanii Kutoka Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama ‘Davido' Ameweza kuwashukuru Watanzania kwa mapokezi waliyompatia pia pamoja na kushare jukwaa moja na Msanii kutoka Marekani T.I amesema hayo kupitia ukurasa wa Istragram pindi alivyokuwa anaondoka nchini Tanzania.
"Kwa heri Tanzania 26464! it was great sharing the stage with trouble man 31...thank you Clouds fm for napkin it possible and bless my brother @diamondplatnumz for welcoming me well" Aliandika DavidoLicha ya kwamba Aliweza kupikwa Mikwara na baadhi ya Vyombo vya Habari vya hapa nchi kuzuiwa kufanya show hiyo.
SOMA ZAIDI >>> »