Pages

Showing posts with label Ajali. Show all posts
Showing posts with label Ajali. Show all posts

Friday, March 13, 2015

BASI LA ARUSHA EXPRESS LAGONGANA NA LORI

 
 

          Basi laArusha express lilillokuwa likitokea mkoani arusha kuelekea Mbeya limepata ajali eneo la kisonga mkoani singida ambapo limegongana na roli
SOMA ZAIDI >>> »

Monday, March 9, 2015

GARI LA SERIKALI LAPARAMIA UKUTA WA SHULE JIJINI DAR

 Gari ya Serikali aina ya Toyota Land Cruser yenye namba za Usajili STK 7278, ikiwa imeparamia ukuta wa Shule ya msingi Al Muntazir iliyopo kwenye makutano ya barabara ya Sea View na Barack Obama Drive,jijini Dar es salaam,mara baada ya dereva wake (jina kapuni) kushindwa kulimudu gari hilo pale alipochomekewa na gari nyingine ambayo iliingia mitini.ajali hii imetokea jioni ya leo,wakati gari hili likiwa linatokea mjini kuelekea Palm Beach.hakuna aliejeruhiwa katika ajali hii.
Wafanyakazi wa "Break Down" wakiangalia namna ya kuichomoa gari hiyo iliyoparamia ukuta wa Shule ya msingi Al Muntazir iliyopo kwenye makutano ya barabara ya Sea View na Barack Obama Drive,jijini Dar es salaam leo.CHANZO MTAA KWA MTAA BLOG
Hivi ndivyo ionekanavyo gari hiyo mara baada ya kuchomolewa kwenye ukuta huo.
Mashuhuda wakitazama gari hiyo.
Gari hiyo ikivutwa na "Break Down" mara baada ya kuchomolewa ukutani
SOMA ZAIDI >>> »

Friday, December 5, 2014

ABIRIA 50 WANUSURIKA KIFO MLIMA NYOKA LEO BAADA YA BASI LA MBUKIO MISSIO KUGONGANA NA LORI

Basi la Mbukio Missio muda mfupi baada ya kupata ajali ambayo ilisababishwa na Dereva wa Basi hilo, Hapa vijana wakiwa wamechukua magazeti wakificha jina la Basi hilo lisitambulike kwa wale wanaokuja kushuhudia ajali hiyo, Nia na lengo la kufanya hivyo haijafahamika mpaka sasa

Lori la Mafuta lenye namba za Usajiri T332 AGA ambalo Dereva wake Godfrey Lyimo (33) alikuwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi, Hapa Lori hilo la mafuta liliwa limepinduka.

Basi la Mbukio Missio Likiwa limeharibika vibaya kwa mbele baada ya ajali hiyo.
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia Ajali hiyo

Baadhi ya Abiria , Washuhudiaji pamoja na Askari wakiwa eneo la Mlima Nyoka ambapo ajali ilipo tokea
Picha na Mbeya yetu Blog.



SOMA ZAIDI >>> »

Thursday, November 6, 2014

BASI LAGONGA TRENI NA KUUWA WATU 12

Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
watu 12 wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi la Super Aljabir linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mahenge mkoani Morogoro kugongana na treni maeneo ya Kiberege karibu na Ifakara, Morogoro jioni hii.

Ajali hiyo imetokea wakati basi hilo likijaribu kuwahi kuvuka reli kabla ya treni kupita.
 
Baadhi ya miili ya watu katika eneo la tukio.

SOMA ZAIDI >>> »