Pages

Friday, April 25, 2014

KONGAMANO LA MAFUTA NA GESI LAZINDULIWA RASMI NA PROFESA MUHONGO MJINI BERLIN,UJERUMANI

 



Waziri  wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifungua kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mada juu ya fursa za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta za mafuta, gesi ikiwa ni pamoja na madini



Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akifungua kongamano hilo

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wajumbe anayewakilisha wafanyabiashara kabla ya kufungua kongamano la  mafuta na gesi linaloendelea huko Ujerumani  kama moja ya   maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na  Zanzibar


Mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini  (TPDC) Bi Venosa Ngowi  (kulia) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye suti nyeusi) shughuli zinazofanywa na shirika hilo kwenye maonesho yanayoendelea huko Berlin, Ujerumani.  Pembeni ya Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo

Mtaalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Nchini (GST) Bi. Augustina Rutaihwa akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) juu  ya shughuli zinazofanywa na wakala huo. Kushoto mwa Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo


Kikundi cha  ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa kongamano hilo

No comments:

Post a Comment