ShabaniKilendemo.blogspot.com inapenda kuungana na watanzania wote wapenda
amani na utulivu kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia
chini ya Viongozi wake wakuu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais
Dk. Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Piter Pinda pamoja na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Alli Mohamed
Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar , Maalim Seif Sharif Hamad, na
Makamu wa pili wa Rais, Balozi, Seif Ali Idd kwa kuulinda na kutuongoza
vyema wananchi wote katika kuulinda na kudumisha Muungano wetu kwa amani
na Utulivu.
Pia
tunawatakia kila la heri watanzania wote popote pale walipo kwa
kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. "TUULINDE
MUUNGANO WETU KWA MAENDELEO, AMANI NA USTAWI WA TAIFA LETU" na daima
tukumbuke "UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU"
No comments:
Post a Comment