Pages

Saturday, April 19, 2014

MADAKTARI WASHINDWA KUUNGANISHA UUME WA MWANAMUZIKI ALIYE JIKATA MAKUSUDI



Rapper mwenye uhusiano na kundi la Wu-Tang Clan, Andre Johnson hana tena kiungo kinachomfanya aitwe mwanaume kwakuwa madaktari wameshindwa kuunganisha.


Mtandao wa TMZ uliandika kuwa Johnson aka Christ Bearer aliukata uume wake jana Jumatano na kujirusha kwenye nyumba ya ghorofa mbili anakoishi huko North Hollywood kwa kile kinachodaiwa kutaka kujiua. Alikimbizwa kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center lakini uume wako umedaiwa kukatika kabisa.

Johnson/Christ Bearer ni member wa kundi liitwalo Northstar, lilioanzishwa na rapper Wu-Tang Clan, RZA. Kulikuwepo na rappers wengine kwenye tukio hilo waliokanusha kuwepo na madawa ya kulevya kiasi cha kumfanya achukue uamuzi huo. Wanaamini kuwa Johnson/Christ Bearer anaweza kuwa na matatizo ya kiakili.

No comments:

Post a Comment