Mbunge wa Nzega Dr. Hamis kigwangwalla
Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangwalla na wenzake 11 wamefikishwa mahakamani wilayani Nzega, mkoani Tabora wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uharibifu wa mali na kufanya mkutano bila kibali.
Mwendesha mashtaka, Merito Ukongoji ambaye ni
mkaguzi msaidizi wa polisi, alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa la
kuharibu mali ya mgodi wa dhahabu wa Resolute yenye thamani ya Sh15.9
milioni.
Pia, alisema watuhumiwa hao ambao walikana
mashtaka yote, wanadaiwa kufanya mkutano bila kibali katika mji mdogo wa
Nzega Ndogo na shtaka la tatu, ni la kufanya maandamano bila kibali,
kitendo kilichodaiwa kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Ukongoji alidai kuwa washtakiwa hao walitenda
matukio hayo Machi 23, mwaka huu katika Kijiji cha Nzega Ndogo na
walikamatwa pembezoni mwa mgodi wa Resolute wakipanga kufanya uharibifu
mkubwa wa mali.
Washtakiwa wengine ni Richard Mayunga, Hamis
Charles, Bernard Bitus, Ibrahim Mrima, Fredrick Mbula, Peter Mandege,
Razalo Shimba, Maganga Seleli, Elikana Daud na Kankoba Sululi na Luhende
Shija.
Mwendesh mashtaka huyo alidai upeleleza
haujakamilika na washtakiwa wapo nje kwa dhamana. Hakimu Mkazi Wilaya,
Joseph Ngomello aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 9, mwaka huu
itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment