Pages

Wednesday, April 30, 2014

MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA LEO ARUSHA


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Richard Sezibera akimkaribisha Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo unaofanyika leo.

 Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha(AICC) kwenye mkutano wa 12 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Arusha.Rais Kenyatta ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wnanachama watano.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijadiliana jambo kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa  wakuu wa nchi za  Jumuiya ya Afrika Masharariki uliofanyika mjini Arusha leo. 

No comments:

Post a Comment