Sagasii alisema hayo kutokana na hoja inayotolewa
na baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba kuwa muundo wa Muungano wa
serikali tatu ni hatari kwa kuwa unaweza kuvunja Muungano.
“Hoja ya kwamba Serikali tatu zitavunja Muungano
hazina mashiko. Mambo yote ambayo yanaonekana kuwa yanaweza kuvunja
Muungano wanayaweka katika Katiba ya Muungano,” alisema Sagasii.
Alisema baada ya kutengeneza Katiba ya Muungano na
Tanganyika nayo itaunda katiba yao ambayo itaainisha masuala
yatakayokuwa ya nchi zao.
Aidha, Sagasii aliyewahi kuwa mkurugenzi wa
shughuli za Bunge, alisema suala la muundo wa serikali limekuwa
likijitokeza mara kwa mara kuanzia mwaka 1984.
Aliwashangaa Wana-CCM kudai kuwa wazo la serikali
tatu linatoka kwa vyama vya upinzani akisema “suala hilo liliibuliwa na
Wabunge wa CCM waliojulikana kama G55 walipotaka kuundwa kwa Tanganyika.
Mbali na Tume ya Jaji Robert Kisanga kuonyesha
mahitaji ya serikali tatu, Sagasii alisema hitaji hilo pia lilionekana
wakati wa utawala wa rais wa pili wa Zanzibar, Abdul Jumbe.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekuwa ya
tano kuibua suala hilo, lakini safari hii ni mwafaka zaidi kwa kuwa
maoni hayo yametokana na wananchi wenyewe.
“Wanaotumia nafasi zao kwa ajili ya kuzuia
serikali tatu ni sawasawa na mpira uliojazwa upepo sasa ukiuzamisha
kwenye maji ukiendelea kuushikilia utabaki katika maji lakini ukiutoa
mkono unaibuka hiyo ndiyo hoja ya Utanganyika,” alisema.
No comments:
Post a Comment