Pages

Sunday, April 20, 2014

PICHA MBALI MBALI KATIKA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA ULIOPIGWA JANA KWENYE DIMBA LA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.


 Mshamuliaji wa Yanga, Simon Msumva (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa Simba, Nassor Chollo (kushoto) na Said Ndemla (katikati) wakati wa mchezo wa kufunga dimba la Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana jioni. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1. 

bao la Simba walioanza kushinda lilifungwa na Haruna Chanongo, katika dakika ya 76 baada ya Krosi safi ya beki William Lucian. Yanga walisawazisha bao hilo katika dakika ya 86 kupitia winga wake machachari, Simon Msuva, kwa shuti kali lililomshinda kipa Ivo Mapunda. hadi mwisho wa mchezo huo, Yanga 1-1 Simba.

 Beki wa Simba, Issa Rashid, akijaribu kumtoka winga wa Yanga, Simon Msuva, wakati wa mchezo huo.

Wachezaki wa Simba, wakishangilia bao lao la kuongoza lililofungwa na haruna Chanongo.
 Simon Msuva, akishangilia bao lake aliloisawazishia Yanga...
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao lao la kusawazisha lililofungwa na Simon Msuva.
 Kikosi cha kwa nza cha Simba na makocha wake....
 Kikosi cha kwanza cha Yanga...

 Mshambuliaji wa Yanga , Hamis Kiiza akiruka kukwepa kwanja la beki wa simba, Nassor Chollo wakati wa mchezo huo. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka wachezaji wa Simba Ramadhan Singano (kulia) na Nassor Chollo.

No comments:

Post a Comment