Young Africans
TAARIFA ZA OKWI, YONDANI, CHUJI HAZINA UKWELI
Uongozi wa klabu ya Young Africans unasikitishwa na taarifa
zinazotolewa na baadhi ya Vyombo Vya Habari siku ya jumatano
kwamba wachezaji Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Athuman Idd "Chuji wamefukuzwa kwenye timu na Emmanuel Okwi ameondoka kurejea kwao nchini
Uganda ni za uongo mtupu.
Hakuna mchezaji yoyote aliyefukuzwa kwenye timu baada ya kupoteza
mchezo dhidi ya Mgambo Shooting mwishoni mwa wiki, taarifa hizo
zinasambazwa kwa Propaganda ili kuweza kuvunja umoja uliopo ndani ya
timu kwa wachezaji na walimu pia kwa Viongozi na wanachama.
Kelvin
Yondani hakuungana na wenzake kambini baada ya kuomba kupumzika na
kutatua matatizo yake ya kifamilia, Benchi la Ufundi walimpa ruhusa hiyo
kwa kuzingatia mchezaji mwenyewe asingeweza kutumika kwa mchezo wa
jumapili dhidi ya JKT Ruvu kufuatia kuwa na kadi tatu za njano,
ataungana na wenzake mara baada ya tu ya mchezo huuo.
Athumani Idd
"Chuji", David Luhende pamoja na kiungo Haruna Niyonzima ni wagonjwa,
wanaendelea na matibabu kuhakikisha wanakua fit na kuungana na wachezaji
wao mara baada ya mchezo wa siku ya jumapili.
Juma Kaseja yupo
kambini pamoja na mlinda mlango Deo Munish "Dida" aliyekua majeruhi kwa
takribani wiki tatu kufuatia kupata jeraha katika mkono wakati timu
ikijiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Emmauel Okwi yupo
jijini Dar es salaam akiendelea na matibabu kufuatia kutonesha goti
katika mchezo dhidi ya Mgambo mwishoni mwa wiki, awali Okwi aliiumia
katika mchezo dhidi ya Prisons na kutolewa nje na machela.
Okwi
akiongea na katibu mkuu wa Yanga Beno Njovu jana ofisini makao makuu ya
Klabu ya Yanga, amesema anaendelea vizuri na ataaungana na wenzake mara
baada ya mchezo wa jumapili, lakini akisikitishwa na habari zilizotolewa
juu yake amabazo hazina ukweli wowote.
Kufuatia
wachezaji hao kushindwa kuungana na timu siku ya jumanne katika mazoezi
ya jioni, kocha mkuu Hans Van der Pluijm alichagua wachezaji 20 ambao
wap kambini kujiandaa na mchezo huo:
Magolikipa: Juma Kaseja, Deo Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barhez"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Ibrahim Job, Raja Zahir ,Oscar Joshua na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Frank Domayo, Said Dilunga, Nizar Khalfani , Salum Telela na Hamis Thabit
Washambuliaji: Hussein Javu, Hamisi Kizza, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu.
Waati
huo huo klabu ya Yanga imewasilisha barua ya malalamiko kwa TFF juu ya
mchezaji Mohamed Hussein Neto kuchezea timu ya Mgambo JKT pasipokuwa na
uhamisho wa kimataifa ITC, kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini,
mchezaji huyo ni raia wa Kongo na jina lake halisi ni Noel Melondoo.
No comments:
Post a Comment