Waombaji wa fursa za ajira Serikalini waliokuwa wametuma maombi ya kazi katika Taasisi mbalimbali za Umma nchini kupitia Sekretarieti ya Ajira wametakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ili kujua endapo wamechaguliwa na kujiandaa kwa ajili ya usaili unaotarajiwa kuanza tarehe 30 Aprili, 2014 hadi Mei 9 mwaka huu.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema hayo wakati akiongea na baadhi ya waajiri waliomtembelea ofisi kwake kwa ajili ya kuzungumza masuala mbalimbali ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Daudi alibainisha kuwa ofisi yake inatarajia kuendesha usaili wa taasisi zipatazo 34 kwa niaba ya waajiri wa taasisi hizo kwa mujibu wa sheria, ambapo alizitaja taasisi hizo kuwa ni Tanzania Library Services Board (TLSB), Ardhi Institute Morogoro, Tanzania Education Authority (TEA), Water Development Management Institute (WDMI), Agency for Development Education Management (ADEM), Tanzania Industrial Research and Development Organization (TIRDO), Ardhi Institute – TABORA, Tanzania Small Holders Tea Development Agency (TSHTDA), Tanzania Institute of Accountancy (TIA), Eastern Africa Statistical Training Centre (EASTC). Dar Es Salaam Maritime Institute (DMI), Institute of Accountancy Arusha (IAA), Tanzania Meat Board (TMB), Tanzania Public Service College (TPSC), The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA),
Taasisi nyingine ni Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), Tanzania Automotive Technology Centre (NYUMBU), College of Business Education (CBE), National College of Tourism Agency (NCT), Dar es salaam Institute of Technology (DIT), Community Development Training Institute (TENGERU), Institute of Finance Management (IFM). Tanzania Electrical Mechanical and Electronics Services Agency (TEMESA), Institute of Adult Education (IAE), Tanzania Investment Centre (TIC), Cashew nut Board of Tanzania (CBT), Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI), College of African Wildlife Management (MWEKA), Tanzania Tourist Board (TTB), Tanzania Airports Authority (TAA), National Institute of Transport (NIT), Local Government Training Institute (LGTI), Institute of Social Work (ISW), Tanzania Tree Seed Agency (TTSA) pamoja na Institute of Rural Development Planning Dodoma (IRDP).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira amewataka waombaji wote waliochaguliwa kufanya usaili kuzingatia masharti ya jumla yaliyotolewa hususani suala la vyeti, tarehe ya usaili, mahali pa kufanyia usaili na muda wa kufanya usaili. Alisisitiza kuwa mtu akikosea na kwenda sehemu nyingine ama kuchelewa muda ajue amejiondoa mwenyewe katika mchakato kutokana na kutokuzingatia maelekezo ya msingi.
Alifafanua kuwa wasailiwa ambao kada zao zimeainishwa kuanza na mtihani wa mchujo (written interview) wasisahau kuangalia tarehe ya usaili wa mahojiano na sehemu usaili utakapofanyikia kama ilivyooneshwa katika tangazo husika la kuwaita katika usaili. Aidha, amewataka wale waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo husika la kuitwa kwenye usaili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na hivyo wasisite kuomba tena kwa mara nyingine pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Alimaliza kwa kusema kuwa taasisi yake itaendesha usaili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili husika kulingana na mahitaji ya waajiri kama walivyoainisha katika vibali walivyowasilisha Sekretarieti ya Ajira.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kwa barua pepe; gcu@ajira.go.tz na Facebook-page ya “Sekretarieti Ajira”
au Tovuti: www.ajira.go.tz na simu 255-687624975
24 Aprili, 2014.
|
Thursday, April 24, 2014
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KWA TAASISI MBALIMBALI
Labels:
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment