Umati uliomsindikiza Aveva kuchukua fomu. |
Aveva akionyesha kadi yake ya uanachama, kulia ni Said Tuliy |
Aveva akikabidhiwa fomu yake ya kugombe Urais |
Alipoingia
alitoa kadi yake ya uanachama kujitambulisha kwa mtoa fomu, kisha
kukabidhi ada na kupewa fomu yake kabla ya kuondoka kwa maandamano
mazito.
Wakati
wa maandamano wanachama walikuwa wakisukuma gari ya Aveva kuanzia
Lumumba hadi makao makuu na mgombea huyo alikuwa akionyesha ishara ya
vidole vitatu, akimaanisha sera yake ni pointi tatu- maana yake ushindi.
Na alipofika makao makuu wanachama ambao walikuwa hapo wakimsubiri nao walimlaki kwa shangwe, wakisema; “Huyu ndiye rais wetu,”.
Kwa ujumla mapokezi ya Aveva
yanaweza kuwakatisha tamaa watu wengine kujitokeza kuwania nafasi hiyo,
kwani Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Usajili ameonekana kuungwa
mkono na watu wengi.
Ni mtu mmoja tu hadi sasa
ambaye tayari amechukua fomu ya Urais mbali na Aveva, ambaye ni Andrew
Tupa, lakini habari zinasema mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo,
Michael Richard Wambura naye atachukua fomu ya nafasi hiyo kesho.
Kihistoria Aveva ni Simba damu
ambaye amekuwa akiisaidia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20 sasa ni
miongoni mwa waasisi wa kundi la Friends Of Simba (F.O.S.), ambalo
limekuwa na msaada mkubwa wa kifedha katika klabu hiyo.
Hajawahi kuwa kiongozi wa
kuchaguliwa, lakini amekwishaongoza kwa mafanikio Kamati kadhaa, ikiwemo
ya Usajili mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambayo ilifanya kazi nzuri ya
kuibua vipaji kama vya akina Boniface Pawasa, Ulimboka Mwakingwe,
Emmanuel Gabriel, Juma Kaseja, Yahya Akilimali, Said Maulid ‘SMG’,
Suleiman Matola na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment