Baadhi
ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B.
Clarke Haulege Construction, Tanki hilo ni mali ya Bw. Bundala Kapela wa
Igunga ni namba T634 BCZ lenye vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita
40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika
barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki
za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto, Jambo
lililomfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya
Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha
na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha
madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea, Katika tukio hilo
lililosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na msururu wa magari
kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliochanganyika na moshi
kutishia usalama wa watumiaji wengine, hata hivyo baada ya moto
kupungua kiasi askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze
kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea na safari, Hakuna mtu
aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo, Angalia matukio
zaidi ya picha hapo chini.
No comments:
Post a Comment