Mwigizaji na muongozaji wa bongomovie Dr. Cheni ambaye alianza kupata
umaarufu kwenye fani ya uigizaji na thamthilia za kundi la Kaole na
sasa akiwa anafanya movie zake, 12 May alizushiwa kifo ikiwa
imeunganishwa na ishu yake ya kulazwa hospitali kutokana na homa ya
dengu.
Baada ya huo uvumi kusambaa Elizabeth Michael ”Lulu” aliandika
>>> ‘Jamani kuna mambo ya kuzushiana lakini sio kifo, kuna
habari zimezushwa kwamba Dr. Cheni amefariki, ni habari za uongo
jamani…. yuko salama kabisa na juzi ameruhusiwa kutoka hospital na
anaendelea vizuri, tunajua kufa ni wajibu lakini mpaka Mungu mwenyewe
apende….. pole baba angu’
Dr Cheni na yeye aliandika ‘Jamani kifo kipo na hakuna atakaekwepa ni
lazima tutakufa na hakuna atakaebakia ila si vyema kunizushia, siku
yangu itafika tu na wote mtajua lakini si jambo la busara kunizushia.
Hii ni moja ya picha zilizosambaa kwenye internet zikimuonyesha Dr Cheni akiwa hospitali
No comments:
Post a Comment