Ujumbe wa Tanzania ukiinua bendera juu kuashiria uwepo wao mkutanoni.
Ujumbe wa Tanzania (waliovaa sare za kijani), kutokakushoto Kanali Martin BusungunaLuteniKanali Joseph Bakari wakati wa mkutano.
Kanali Busungu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya ya Baraza.
Luteni Kanali Bakari akichangia mada wakati wa Mkutano
JWTZ limeshirikiMkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa (General Assembly and Congress of the International Military Sports Council -CISM) uliofanyikaMjini Quito, EquadoAmerica ya Kusinikuanziatarehe 05-09 Mei, 2014.
Mkutano
huo ulijadilina kuendelea kusikiliza na ushiriki wa majeshi katika
Michezo ya Kimataifa chini ya Kauli mbiu ya Baraza hilo isemayo Urafiki
kupitia Michezo (Friendship through sports), msisitizo ukiwa katika
kutumia michezo kama chombo cha kueneza amani na utulivu kati ya mataifa
duniani.
Badala
ya kukutana na kushirikiana katika maeneo ya vita na migogoro, majeshi
yakutane katika michezo na kujenga uelewano na mashirikiano
yatakayopunguza uwezekano wa kuingia katika vita kama njia ya kutatua
migogoro.
Moja
ya mambo yaliyojitokeza katika mkutano huo ni pamoja na ushiriki mdogo
wa nchi za Afrika ikilinganishwa na mabara mengine, uliodaiwa kutokana
na kukosekana fedha, mwamko mdogo wa viongozi wa majeshi ya nchi husika
na kutoona umuhimu wa kujenga mahusiano kupitia michezo.
Aidha,
Mkutano ulimchagua Rais mpya wa Baraza hilo, Kanali Abdul Hakeem kutoka
Bahrain na Kanali Dorah Mumby (Guinea) kuwa Katibu Mkuu wa kwanza
kutoka Afrika.
Ushiriki
wa Tanzania na utekelezaji wa maazimio ya CISM umekuwa wa mfano kwa
miaka kadha sasa. Kwa mfano,katika mkutano wake wa mwaka 2008
uliofanyika Paramaribo, Suriname, Meja Joseph Bakari (sasa Luteni
Kanali) alitunukiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza hilo Nishani
iitwayo ‘Order of Grand Knight’ kwa mchango wake uliopelekea kuanzishwa
kwa “Twalipo Youth Sports Foundation”
Katika
mkutano huojumla ya wanachama 76 walihudhuria kati ya wanachama 104 wa
Baraza hilo. Tanzania iliwakilishwa na Kanali MartinBusungu, Mkurugenzi
wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni kutoka Makao Makuu ya Jeshi na
LuteniKanali Joseph Bakari, Afisa mnadhimu kutoka Kurugenzi hiyo.
Mkutano
huo wa mwaka hutanguliwa na mikutano ya kimabara (Afrika, Ulaya,
AsianaAmerika) ambako masuala ya michezo ya Majeshi yanayogusa mabara
husika hujadiliwa.kutoka
ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya ushirikiano Kusini mwa Afrika
nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda na Zambia.
No comments:
Post a Comment