Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia
salamu za rambirambi mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
FECOFA, Omar Constant kutokana na vifo vya washabiki.
Washabiki
12 walipoteza maisha uwanjani wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo
kati ya TP Mazembe na AS Vita iliyochezwa kwenye Uwanja wa Tata Raphael,
jijini Kinshasa.
“Tumeguswa
na msiba huo mzito, tunatoa salamu za rambirambi kwako (Rais wa
FECOFA), familia za marehemu pamoja na wadau wote wa mpira wa miguu
katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,” imesema sehemu ya barua hiyo ya
Rais Malinzi.
No comments:
Post a Comment