Pages

Thursday, May 15, 2014

MATUKIO MBALI MBALI KWENYE ZIARA YA KINANA WILAYANI SIKONGE,TABORA

 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopata umeme chini ya mradi wa umeme vijijini katika wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Sikonge mkoani Tabora. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Sikonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM  Sikonge ambapo aliwapongeza kwa juhudi zao za kuleta maendeleo yao katika ngazi ya wilaya lakini pia alisema wakulima wanatakiwa kusaidiwa mara moja kuondoa kero zao. 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wakazi wa wilaya ya Sikonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM  Sikonge . 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua Album ya kikundi cha Kwaya cha Umoja Sanaa Group chenye wasanii 27 ambao wanaimba nyimbo za kuhamasisha Chama cha Mapinduzi wilayani Sikonge mkoa wa Tabora.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Sikonge ambapo aliwaambia wawe makini sana na sera za vyama vya upinzani  kwani vyama vingine sera zao si nzuri kwa maendeleo ya Taifa 
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tabora Mwanne Nchemba akiwasalimu wakazi wa Sikonge kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndgu Abdulrahman Kinana uliofanyika Sikonge mkoani Tabora.
 Wasanii wa Kikundi cha Umoja Sanaa Group wakitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia wakazi wa Sikonge mkoani Tabora .

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma orodha ya nyimbo zilizopo kwenye album ya kikundi cha Umoja Sanaa Group cha CCM Sikonge,kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ndugu Fatma Mwassa akiangalia kasha la album hiyo na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .

No comments:

Post a Comment