Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye viwanja vya mkutano
Gombani ya Kale akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (ZNZ) Ndugu Vuai
Ali Vuai tayari kwa kuhutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (ZNZ) Vuai Ali Vuai akihutubia wananchi wa Pemba kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wananchi wa mikoa miwili ya Pemba katika viwanja vya Gombani ya Kale.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba na kuwataka kuwa makini na viongozi wenye kauli mbili mbili kwani hawana nia njema na maendeleo yao zaidi ya kujifikiria wao binafsi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi kwenye viwanja vya mikutano vya Gombani ya Kale,Pemba na kuwaambia wananchi hao kuwa CCM itaenda sambamba na wapotoshaji wa ukweli.
Wananchi wakionyesha ishara ya muundo wa Serikali mbili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Gombani ya Kale,Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka na Viongozi wengine wa CCM Zanzibar wakionyesha ishara ya muundo wa Serikali mbili za Muungano wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Gombani ya Kale.
Mabinti wa UVCCM Pemba wakisoma utenzi wa kumkaribisha KatibuMkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kutoka kushoto ni Fatuma Juma Ramadhani na Halima Juma Haji kwenye viwanja vya Gombani ya Kale.
Sheikh Hamisi Ali Hamisi akisoma dua kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Gombani ya Kale Pemba ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia umati.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka akihutubia wakazi wa Pemba na kuwaambia wawe makini na viongozi wanafiki wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment